Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION PAMOJA NA TIBA YAKE



DEPRESSION

• • • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION PAMOJA NA TIBA YAKE


Tatizo la depression huhusisha hali ya mtu kuwa na huzuni kubwa,kuhisi hasira na kuhisi kupoteza kila kitu hali ambayo hupelekea hadi kushindwa kufanya kazi zake za kila siku,na tafiti zinaonyesha tatizo hili huzidi zaidi kwa watu wenye matatizo kama vile;


- Asthma

- Magonjwa ya moyo

- Tatizo la arthritis

- Kansa au Saratani

- Tatizo la kisukari

- Unene au uzito kupita kiasi yaani obesity n.k


DALILI ZA TATIZO LA DEPRESSION NI PAMOJA NA;


1. Mtu kuhisi huzuni,kupoteza tumaini,hasira,kutokutulia,au hofu mara kwa mara


2. Mwili kuchoka kupita kawaida,kuhisi kushindwa kufanya kila kitu, kushindwa kukocentrate au kufocus kwenye kile unachokifanya, wengine kuanza kulewa sana pombe, kutamani kujitoa uhai n.k


3. Tatizo la depression pia huweza kusababisha tatizo la mtu kuanza kupoteza kumbu kumbu(memory loss)


4. Kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri na kufanya maamuzi sahihi kila mara


5. Mtu kupoteza kabsa interest ya kile kitu anachokifanya na kutamani kuacha kabsa kuendelea


6. Mtu kujiona mkosaji kila mara,na wengine hupenda kuomba msamaha kila mara hata kwa vitu ambavyo kwa hali ya kawaida ni sahihi


7. Mtu kujihisi mpweke,kupenda kukaa mwenyewe na kujitenga na watu, kuhisi aibu mbele za watu kila mara


8. Mtu kupoteza kabsa hamu ya kula chakula hali ambayo hupelekea kukonda sana na kuwa na uzito mdogo wa mwili


9. Mtu kufikiria kujiua au kujidhuru mara kwa mara


10. Mtu Kuwa na tatizo la kukosa usingizi


11. Mtu kuanza kupatwa na tatizo la maumivu makali ya kichwa, Tumbo pamoja na mgongo


12. Baadhi yao huanza kupatwa na matatizo kama vile kuharisha mara kwa mara,kichefuchefu na kutapika


13. Kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa au kushindwa kufanya tendo la ndoa n.k


CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION


- Family history, kama kwenye familia yenu kuna mtu mwenye tatizo kama hilo uwezekano wa wewe kupatwa pia ni mkubwa


- Kukutana na matatizo mbali mbali katika umri mdogo kama vile ajali,vifo n.k


- Mtu kuwa na matatizo mbali mbali kwenye ubongo wake kama vile sehemu ya mbele ya ubongo yaani frontal lobe kuwa less active n.k


- Kukutana na matukio magumu kwenye maisha yako kama vile; kufukuzwa kazi,kufeli mitihani kwa wanafunzi, matatizo ya ndoa,mahusiano n.k


- Matatizo mbali mbali ya kiafya kama vile; tatizo la kukosa usingizi(insomnia),kisukari,presha,asthma n.k


- Matumizi ya vilevi kama pombe,uvutaji wa sigara n.k 


MATIBABU YA TATIZO LA DEPRESSION


Kuna njia mbali mbali hutumika kumsaidia mtu mwenye tatizo la depression kama vile;


• Kufanya mazoezi ya mwili kila siku angalau kwa dakika 30 au nusu saa


• Kula vyakula vyenye virutubisho vyote


• Kuepuka unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara


• Kujifunza kusema "HAPANA" kwa kila unachokiona kinaenda tofauti na ilivyo kawaida


• Pata msaada wa kisaikolojia yaani psychotherapy kama kuna huduma kama hiyo eneo ulilopo


• Pata muda wa kutosha wa kupumzika,kurefresh mind,kuongea na watu tofauti tofauti wala usikae peke yako, pamoja na muda wa Kulala


• IBADA, Tafiti zinaonyesha Ibada imeonekana kuwa tiba kuu ya tatizo hili,hivo kama ni mkristo au muislam nenda sehemu za ibada hudhuria sana kila kipindi,hali hiyo itaisha na kukujengea tumaini jipya la maisha


• Kwa upande wa Dawa, kuna dawa mbali mbali kama vile;


✓ Antidepressants mfano; Fluvoxamine(Luvox)


✓ Antiaxiety mfano; Diazepam


✓ Antipyschotic N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments