KIKOHOZI
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUKOHOA MFULULIZO
Tatizo hili la mtoto kukohoa mfululizo huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile kuharisha,kutapika,homa n.k
Je nini chanzo cha shida hii kwa watoto? na kitu gani cha kufanya ikiwa mtoto wako ana shida hii? soma hapa kwenye makala hii..!!
CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUKOHOA MFULULIZO
Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia uwepo wa shida hii kwa watoto kama vile;
1. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama bacteria,fangasi,au virusi kwenye mfumo mzima wa koo la hewa.
2. Mtoto kuwa na Tatizo la acid kupanda kutoka tumboni yaani kwa kitaalam ACID REFLUX huweza kusababisha mtoto kuanza kukohoa mfululizo, kutapika mara kwa mara,kupatwa na kiungulia n.k
3. Mtoto kuwa na ugonjwa wa asthma
4. Mtoto kuwa na tatizo la Allergies(mzio) juu ya vitu mbali mbali kama vumbi, marashi, n.k
Hali hii huweza kuambatana na kikohozi cha mfululizo, kuwashwa kooni, kutokwa na machozi, kuanza kupata upele kwenye ngozi au rashes, pua kuvimba n.k
5. Mtoto kuwa na ugonjwa wa Kifaduro ambapo kwa kitaalam hujulikana kama whooping cough au Pertussis.
6. Pamoja na sababu zingine kama vile; matatizo ya kurithi baadhi ya vinasaba vya tatizo hili katika ukoo au familia flani n.k
UKIONA MTOTO ANA DALILI KAMA HIZI HAPA CHINI AWAHI HOSPITALINI
- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la kushindwa kupumua au kukosa pumnzi
- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la kupaliwa kila mara
- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la mtoto kutapika mfululizo
- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la uchovu wa mwili kupita kiasi,mwili kukosa nguvu n.k
- Kikohozi ambacho kinaambatana na shida ya kubadilika rangi kwa ngozi kwenye lips za mdomo pamoja na kucha kuwa Blue
Mtoto anatakiwa kwenda hospital kwa ajili ya vipimo ili kupata tiba sahihi kulingana na chanzo cha tatizo lake.
KIKOHOZI HIKI HUWEZA KUAMBATANA NA SHIDA ZINGINE KAMA VILE:
✓ mtoto kupiga chafya mara kwa mara
✓ mtoto kuchoka sana
✓ mtoto kuvimba pua
✓ mtoto kuwa na homa
✓ mtoto kukosa kabsa hamu ya kula chakula
✓ mtoto kuharisha
✓ mtoto kutapika
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!