TEZI DUME
• • • • • •
DALILI ZA TEZI DUME PAMOJA NA MATIBABU YAKE(wanaume)
Prostate ni tezi/kiungo cha kipekee cha kiume, Tezi ya Prostate ipo chini ya kibofu cha mkojo na inaunganisha na uume. Kazi yake ni kutoa sehemu ya maji ya semen ambayo ni ya alkali, ambayo husaidia kuongeza urefu wa maisha ya shahawa inapoingia ndani ya uke.
Prostate pia ina misuli ya hiari ambayo husaidia kutoa shahawa wakati wa kumwaga.
Katika Hali flani kwa wanaume kadri umri unavyokuwa mkubwa na kuzeeka huweza kupatwa na tatizo la benign prostatic hypertrophy (BPH au prostate iliyozidi).
Urethra ni mfereji ambao hupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo. Mwanamume mwenye tatizo la benign prostatic hypertrophy(BPH) mara nyingi huwa na shida ya kutoa mkojo kwa sababu urethra inabanwa na tishu za kibofu.
Ukandamizaji huu hufanya iwe ngumu kwa kibofu cha mkojo kutoa shinikizo la kutosha Kwa wakati, na kibofu chenyewe huanza kudhoofika na kufanya iwe vigumu zaidi kwa mkojo kutoka.
DALILI ZA TEZI DUME PAMOJA NA MATIBABU YAKE(wanaume)
Dalili za BPH ni pamoja na:
- Mwanaume kuanza kukojoa mara nyingi zaidi
- Mkojo kutoka kwa Uharaka zaidi na kushindwa kujizuia,hali ambayo huweza kusababisha mwanaume kujikojolea
- Kusita kwa mkojo; Mwanaume kupata shida ya kugoma kwa mkojo,wakati anataka kukojoa
- Mwanaume Kutumia nguvu zaidi wakati wa kukojoa
- Mkojo kutoka kwa kiasi kidogo sana
N.k
MATIBABU YA TEZI DUME
Matibabu ya BPH huweza kujumuisha dawa au upasuaji inategemea na tatizo lilivyo kwa mtu, Hivo mtu mwenye shida hii anatakiwa awahi hospital kwa ajili ya kupata vipimo pamoja na Matibabu.
• Soma kwa kina hapa: Kuhusu Ugonjwa wa Tezi Dume,Maana,Chanzo,Dalili Pamoja na Tiba yake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!