DALILI ZA UKOMO WA HEDHI(Menopause)

HEDHI

• • • • •

DALILI ZA UKOMO WA HEDHI(Menopause)


 Mwanamke ambaye amekaribia ukomo wa hedhi(perimenopause), anaweza kupata dalili  mbali mbali na dalili hizo ni kama vile:


-Blid kuanza kutokueleweka kama mwanzoni


 - Kuanza kupata tatizo la Ukavu wa uke


 - Mwili Kuwaka moto au kuwa na joto sana kuliko kawaida


 - Kuhisi Baridi sana mara kwa mara


- Mwili Kutoa sana Jasho wakati wa usiku


- Kuanza kukosa usingizi au kupata Shida ya kulala


 - Mood hubadilika


 - Kuongezeka kwa uzito wa mwili na kupungua kwa mchakato wa kimetaboliki


- Kuwa na Nywele nyembamba na ngozi kavu


- Kupoteza umbo la matiti,matiti kusinyaa zaidi n.k


- Ishara na dalili, pamoja na mabadiliko katika hedhi vinaweza kutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine.  


 Vipindi vya kuanza kukosa hedhi mara kwa mara kuliko ilivyokawaida vinatarajiwa kutokea.  Mara nyingi, vipindi vya hedhi vitaruka mwezi na kurudi, au kuruka miezi kadhaa na kisha kuanza mizunguko ya kila mwezi tena kwa miezi michache. 


 Vipindi hivi pia huweza kuhusisha kutokea kwa mizunguko mifupi,  Licha ya vipindi visivyo vya kawaida, ujauzito pia unawezekana katika kipindi hiki.  Hivo ni muhimu pia kuchukua tahadhari kwani uwezo wa mwanamke kutokubeba mimba huanza baada ya kuingia kipindi cha ukomo wa hedhi na sio karibu na ukomo wa hedhi.


Kwa maana nyingine,mwanamke ambaye amekaribia ukomo wa hedhi anaweza kubeba mimba pia.

 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!