Connect with us

afyatips

AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO PAMOJA NA FAIDA ZAKE

Published

on

MJAMZITO

• • • • • •

AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO


Nidhahiri kwamba mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito,lakini yapi ni mazoezi salama kwa mama mjamzito,Baadhi ya wakina mama wajawazito hushauriwa sana kuhusu kufanya mazoezi lakini hawaambiwi ni aina gani ya mazoezi ambayo ni salama kwao, Na kama ni hivo basi,kwa tafsri nyingine kuna mazoezi ambayo sio salama kabsa kwa mama mjamzito.


AINA YA MAZOEZI AMBAYO NI SALAMA KWA MJAMZITO NI PAMOJA NA;


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kutembea


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuogelea au Swimming


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli ambayo imesimama(Riding a stationary bike), hapa nitoe angalizo: ni hatari sana kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuendesha baisikeli inayotembea hasa ya magurudumu mawili tu,kwani ni rahisi sana kukosa balance na kudondoka hivo kuhatarisha ujauzito aliyobeba.


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya YOGA, mazoezi haya ni mazuri japo yanatakiwa kufanyika chini ya usimamizi wa wataalam yaani Instructor, kwani endapo mama atafanya mazoezi ya Yoga ambayo huhusisha zaidi kulalia Tumbo lake au kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First trimester huweza kuwa sio salama kwake.


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo mbali mbali vya mwili, Wakati wa kufanya mazoezi epuka kunyanyua vitu vizito sana


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kukimbia


– Mama mjamzito kufanya mazoezi ya kuruka kamba pamoja na vitu vingine mbali mbali, hapa pia ni muhimu kufanya mazoezi haya kwa msaada wa wataalam au Instructor kuhusu jinsi ya kuruka kamba taratibu,kwa sababu wapo ambao wameruka kamba sana na pia wakapata madhara kwenye ujauzito wao.


Hutakiwi kufanya mazoezi ya kuruka sana au kuruka kupita kiasi, hivo uangalifu mkubwa hutakiwa katika aina hii ya mazoezi Pamoja na mazoezi mengine ambayo sikuyataja hapa,


ANGALIZO: zingatia mambo haya wakati unafanya mazoezi


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kugandamiza tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia mgongo kwa muda mrefu hasa baada ya miezi mitatu ya ujauzito yaani First tremester


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kulalia tumbo sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha mtikisiko mkubwa sana wa tumbo


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kunyanyua vitu vizito sana


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kubana pumzi yako


• Epuka kufanya mazoezi yanayohusisha kuruka sana kupita kiasi


• Epuka kufanya mazoezi ya kucheza mpira kama vile mpira wa miguu wakati wa ujauzito

 N.k


FAIDA ZA MAMA MJAMZITO KUFANYA MAZOEZI


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia sana kuleta mzunguko mzuri wa damu kwenye mishipa ya damu,kwenye moyo pamoja na mapafu


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia ongezeko la uzito ambao hutakiwa kwa mama mjamzito


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na matatizo mbali mbali kama vile;


   • Kupatwa na tatizo la Kukosa pumzi


   • Kupatwa na tatizo la choo kigumu


   • Kupatwa na tatizo la kiungulia kikali


   • Kupatwa na tatizo la kuvimba miguu 


    • Kupatwa na tatizo la maumivu ya mgongo,misuli ya mwili 


     • Kupatwa na tatizo la mishipa ya damu kuvimba au Varicose veins N.k


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito humsaidia mama mjamzito kupata usingizi wakati wa kulala


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa matatizo kama vile kisukari wakati wa ujauzito yaani Gestational diabetes,kifafa cha mimba n.k


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia kupunguza uwezekano wa mama mjamzito kujifungua kwa upasuaji


– Kufanya Mazoezi wakati wa ujauzito husaidia mama kuandaa mwili wake na labor,hata kupelekea urahisi wa mtoto kushuka,njia kufunguka na mama kuwa na pumzi ya kutosha wakati wa kusukuma mtoto.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

afyatips

Dalili za uric acid kuzidi mwilini,Fahamu hapa

Published

on

Dalili za Uric Acid Kuzidi Mwilini, Ishara, Takwimu na Vyanzo vyake

Uric acid ni taka inayozalishwa mwilini baada ya kuvunjwa kwa kemikali zinazoitwa purines, ambazo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula na pia hutengenezwa na mwili. Kwa kawaida, uric acid hutolewa kupitia figo kwa njia ya mkojo. Hata hivyo, kiwango chake kinapozidi (hyperuricemia), kinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Takwimu duniani

  • Tafiti zinaonyesha kuwa takriban asilimia 20 ya watu wazima duniani wana kiwango cha juu cha uric acid, ingawa wengi hawana dalili mwanzoni.
  • Kati ya watu wenye uric acid nyingi, karibu asilimia 20–25 wanaweza kupata ugonjwa wa gout katika maisha yao.
  • Ugonjwa wa gout unaathiri zaidi ya watu milioni 55 duniani, na idadi inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Dalili za uric acid kuzidi mwilini

1. Maumivu makali ya viungo

Dalili maarufu zaidi ni maumivu ya ghafla kwenye viungo, hasa kidole kikubwa cha mguu. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kushindwa kutembea.

2. Kuvimba na wekundu wa kiungo

Kiungo huvimba, huwa chekundu na kuwa cha moto au kupata hali ya joto/kuhisi kuungua kutokana na mkusanyiko wa uric acid.

3. Kiungo kuwa kigumu kusogeza

Baada ya shambulio la gout, kiungo kichoathirika kinaweza kuwa kigumu kukunja au kunyoosha. Mfano Kidole cha Mguu au Kidole cha Mkono n.k.

4. Maumivu ya mara kwa mara hasa usiku

Mashambulizi mengi ya gout hutokea usiku na yanaweza kumwamsha mtu usingizini.

5. Vinundu chini ya ngozi (Tophi)

Kwa watu wenye uric acid nyingi kwa muda mrefu, hujitokeza vinundu vigumu kwenye vidole, masikioni, mikononi au kwenye viwiko.

6. Mawe kwenye figo(Kidney stones)

Uric acid nyingi inaweza kuathiri figo zako kwa njia mbali mbali ikiwemo kutengeneza mawe kwenye figo(kidney stones) na kusababisha:

  • Maumivu makali ya mgongo au ubavu.
  • Kukojoa Damu kwenye mkojo.
  • Maumivu wakati wa kukojoa.n.k.

7. Kupungua uwezo wa figo kufanya kazi

Iwapo hali itaendelea bila matibabu, inaweza kuharibu figo polepole.

Nini husababisha uric acid kuongezeka?

  • Kula nyama nyekundu kwa kiwango kikubwa na maini mara kwa mara.
  • Kunywa pombe, hasa bia.
  • Vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Unene uliopitiliza.
  • Kuwa na Ugonjwa wa figo.
  • Kuwa na matatizo kama vile Kisukari na shinikizo la damu.
  • Kutumia Baadhi ya dawa kama jamii ya diuretics.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

  • Wanaume.
  • Wanawake baada ya kukoma hedhi.
  • Wenye historia ya gout kwenye familia.
  • Watu wenye uzito mkubwa.
  • Wenye magonjwa ya figo au kisukari.

Jinsi ya kupunguza uric acid

  • Kunywa maji ya kutosha kila siku.
  • Punguza nyama nyekundu na vyakula vyenye purines nyingi.
  • Epuka pombe na vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Punguza uzito ikiwa una uzito uliopitiliza.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara.
  • Tumia dawa ulizoandikiwa na daktari ikiwa kiwango ni cha juu au una gout.

Bonus point;

Uric acid nyingi mwilini inaweza isiwe na dalili mwanzoni, lakini ikiachwa bila kudhibitiwa inaweza kusababisha gout, mawe kwenye figo na hata uharibifu wa figo. Ukipata maumivu makali ya viungo, hasa kwenye kidole kikubwa cha mguu, ni muhimu kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema.

Je,Unachangamoto hii? Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.

Reference;

Continue Reading

afyatips

Njia 11 za Kupunguza Cortisol Kiasili

Published

on

Njia 11 za Kupunguza Cortisol Kiasili

Makala hii inaeleza jinsi cortisol (homoni ya msongo wa mawazo) inavyoongezeka wakati wa stress na jinsi inaweza kuathiri afya—ikiwemo kuongeza hatari ya sonona (depression), kuongezeka uzito, tatizo la kukosa usingizi na uchovu mwingi mwilini. Kisha inatoa njia za asili za kuipunguza.

Kazi ya Cortisol

Cortisol ni homoni muhimu inayosaidia:

  • Kudhibiti shinikizo la damu
  • Kudhibiti mzunguko wa usingizi
  • Mwili kukabiliana na Msongo wa mawazo(stress),hatari mbali mbali n.k

Lakini inapokuwa juu kwa muda mrefu → huongeza matatizo ya afya.

Njia 11 za Kupunguza Cortisol Kiasili

1. Kufanya Mazoezi ya mwili

Fahamu kufanya Mazoezi hupunguza stress na kuongeza homoni za furaha kama serotonin na endorphins.

2. Kutumia muda nje

Siri ambayo wengi hawaijui,Kutembea kwenye mazingira ya kijani au mazingira kama ya bustani kwa dakika 20–30 hupunguza cortisol kwa haraka.

3. Lishe bora

Chagua lishe au chakula unachokula kwa Makini Zaidi:

  • Kula vitu kama;Mboga, matunda
  • Samaki kama salmon
  • Karanga, mafuta ya mzeituni
  • Epuka: sukari, caffeine nyingi, na pombe

4. Fanya Zoezi la Kupumua kwa kina (deep breathing)

Kupumua taratibu kwa mpangilio maalum hupunguza msongo na kutuliza mwili.

5. Mahusiano mazuri

Kuwasiliana na marafiki hupunguza upweke, ambao huongeza cortisol.

6. Grounding techniques

Kukaa kwenye “present moment” kama:

  • Kufanya stretching
  • Kusikiliza muziki
  • Kufanya meditation fupi

7. Kicheko,je hii nayo ni dawa? Ndyo

Kucheka kunaweza kupunguza cortisol hadi karibu 40%.

8. Usingizi bora

Kukosa Usingizi huongeza cortisol; hivyo kulala vizuri ni muhimu sana kwa afya yako.

9. Kupunguza stress kwa njia mbalimbali

Fanya Vitu unavyovipenda sana,kama kusikiliza muziki,kuandika journal, kutembea au kufanya mazoezi.

10. Mwendo wa mwili (movement)

Kila aina ya shughuli (kutembea, kazi za nyumbani) n.k husaidia kupunguza stress.

11. Mapumziko kazini au shuleni

Kupumzika kila saa chache husaidia ubongo kurefresh na kupunguza stress.

Kumbuka;

Cortisol ikizidi kwa muda mrefu inaweza kuathiri afya ya akili na mwili. Lakini mabadiliko madogo ya maisha kama:

  • mazoezi,
  • usingizi mzuri,
  • lishe bora,
  • na kupunguza stress

yanaweza kuisaidia mwili kurudi kwenye hali ya utulivu.

Continue Reading

afyatips

Hiki ndicho kinachotokea kwa mtu anayevuta sigara

Published

on

🚬 Hiki ndicho kinachotokea kwa mtu anayevuta sigara…
Mwili huanza kuathirika taratibu, lakini madhara yake huwa makubwa kadri muda unavyopita. Madaktari wanaeleza kuwa sigara huingiza kemikali zaidi ya 7,000 mwilini, nyingi zikiwa hatari kwa mapafu, moyo na ubongo.
Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha: 
• Saratani ya mapafu, koo na mdomo
• Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo
• Kupungua kwa uwezo wa kupumua
• Uharibifu wa meno na fizi
• Uraibu wa nikotini unaofanya kuacha kuwa ngumu
Wataalamu wa afya pia wanaonya kuwa moshi wa sigara unaathiri hata watu wasiovuta waliopo karibu na mvutaji.
Kadri mtu anavyoendelea kuvuta sigara, ndivyo mwili unavyozeeka haraka na hatari ya kupata magonjwa makubwa kuongezeka.
Vyanzo: Shirika la Afya Duniani (WHO), Centers for Disease Control and Prevention (CDC), pamoja na U.S. Food and Drug Administration (FDA).
Continue Reading

Trending

Copyright © 2017 Zox News Theme. Theme by MVP Themes, powered by WordPress.