MTOTO
• • • • • •
HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO BAADA YA KUZALIWA
Zifahamu hatua mbali mbali za ukuaji kwa mtoto(Stages of development) au kwa kitaalam zaidi hujulikana kama Developmental milestones, Hatua hizi za ukuaji zinahusisha mtoto mwenye afya bora ambaye hana tatizo lolote ambalo linaweza kuchelewesha ukuaji wake.
Fahamu kwamba matatizo kama vile; Utapiamlo, upungufu wa baadhi ya vichocheo au hormones mwilini, matatizo ya Ubongo,mtoto kukosa hewa ya kutosha ya oxygen kwenye ubongo n.k vyote hivi huweza kuchelewesha ukuaji na maendeleo ya mtoto wako
Tangia mtoto anazaliwa mpaka anakuwa mtu mzima kuna hatua mbali mbali za ukuaji ambazo anazipitia huku zikihusisha mambo mbali mbali kama vile mabadiliko ya mwili,tabia n.k
HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO BAADA YA KUZALIWA
Kwa kawaida mtoto huzaliwa na kichwa chenye mzunguko wa sentimita 35 na kuongezeka sentimita moja kila mwezi na baada ya miezi 12 kichwa hufikisha sentimita 46
2. WIKI YA SITA BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Katika kipindi hiki au umri huu mtoto huendelea kupata mabadiliko mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kutabasamu pasipo kuongea kitu chochote.
3. MWEZI WA PILI BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Kwenye mwezi wa pili, mtoto huanza kukunja na kunyoosha mikono huku akivuta nguo zake na za mtu mwingine aliyembeba.
4. MWEZI WA NNE BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Mtoto anapofikisha umri wa miezi minne huanza kushika vitu na kuviweka mdomoni na kuanza kugeuka pale anaposikia sauti ya mtu inaita na kuweza kutumia shingo yake vizuri zaidi.
5. MWEZI WA SITA BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Katika kipindi hiki mtoto huendelea kupata mabadiliko mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na kuanza kuota meno, kuanza kutambaa, kuanza kukaa mwenyewe na kupata wasiwasi akimuona mtu ambaye hamfahamu.
6. MWEZI WA TISA BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Kwenye mwezi wa tisa; mtoto huanza kusimama mwenyewe na kuanza kuita majina mbali mbali kama vile mama,baba,dada, kaka na kuanza kucheza michezo ya kitoto.
7. MWEZI WA 12 BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Baada ya mtoto kufikisha umri wa mwaka mmoja toka azaliwe yaani miezi 12, ndipo huanza kutembea mwenyewe kwa kukusaidiwa na vitu mbali mbali baada ya kuvishika au kwa kushikwa na mtu japo baadhi ya watoto wengine huwahi zaidi kuanza kutembea hata kabla ya mwaka kuisha.
8. MWEZI WA 15 BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Mwezi wa 15 mabadiliko mbali mbali huendelea kutokea ikiwa ni pamoja na uwezo wa mtoto kutembea mwenyewe, Mtoto kuweza kuchora mstari na kuonyesha kitu anachokihitaji kwa kidole pamoja na vitu vingine.
9. MWEZI WA 18 BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Hapa mtoto huweza kupanda ngazi, huongeza idadi ya maneno na hufuata akiagizwa kufanya au kutofanya kitu fulani, hapa huanza kutumia kijiko na kujishika sehemu za mwili wake.
10. MIAKA MIWILI(2) BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili, huweza kufanya vitu vingi zaidi kama vile; kukimbia na kupiga mpira, huweza kuvua nguo na kuanza kutamka maneno kama mimi, wewe yule na kadhalika.
11. MIAKA MITATU(3) BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Umri wa miaka mitatu tayari mabadiliko makubwa yameshatokea mwilini na bado yanazidi kutokea hapa mtoto anazidi kua mkubwa na kuanza kusimama kwa mguu mmoja, kukimbia zaidi, kujua jinsia na umri wake, huweza kuvaa na kuvua nguo lakini hawezi kufunga vifungo, anaweza kuhesabu moja mpaka kumi kama akifundishwa, anaweza kuruka na kuchora duara.
12. MIAKA MINNE(4) BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Mtoto mwenye umri wa miaka minne huweza kufanya mambo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuweza kusimulia kitu kilichomtokea,kufunga vifungo vya shati mwenyewe,kuweza kutumia choo mwenyewe na kwenda kujisaidia bila shida yoyote, Kuweza kucheza michezo mingi zaidi, kuweza kuruka kwa mguu moja bila kuanguka n.k.
13. MIAKA MITANO(5) BAADA YA MTOTO KUZALIWA
Katika umri huu wa miaka mitano; mtoto anaweza kuzitambua rangi nne za msingi, anaweza kuendesha baiskeli, anaongea kama watu wengine bila kuchanganya wakati uliopo na ujao,uelewa na akili yake kuzidi kukua zaidi pamoja na kufanya mambo mengine mengi sana.
Hizo ndyo baadhi ya Hatua za Ukuaji wa mtoto toka anazaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!