UUME
• • • • •
KANSA YA KWENYE UUME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Kansa ya Uume, ni ukuaji wa seli usio wa kawaida na usiodhibitika ndani ya uume ambapo kwa asilimia kubwa huanza kwenye seli za ngozi ya uume kisha kuingia ndani,
Bila shaka aina hii ya kansa ya Uume itakuwa haitajwi sana kama aina zingine za kansa kwa wanaume kama vile kansa ya Tezi dume n.k, lakini kansa hii ipo na inapata baadhi ya Wanaume pia.
CHANZO CHA KANSA YA UUME
- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa aina hii ya Kansa,japo kutokana na tafiti mbali mbali imeonekana Kansa ya Uume hupata sana makundi haya yafuatayo;
1. Wanaume wenye kirusi cha HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)
2. Wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60
3. Wanaume wanaovuta sana Sigara
4. Wanaume wenye kinga ndogo ya mwili kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya UKIMWI au matumizi ya baadhi ya dawa n.k
5. Wanaume ambao hawajatahiriwa,ambapo maji maji pamoja na uchafu unaojulikana kama "smegma" hujikusanya chini ya ngozi ya uume na kukuweka katika hatari zaidi
6. Mwanaume kuwa na tatizo la phimosis ambapo ngozi ya uume hushikamana zaidi na kukakamaa hali ambayo hupelekea kuwa vigumu kusafishwa vizuri
7. Mwanaume kuwa kwenye matibabu ya psoriasis pamoja na matumizi ya dawa za psoralen au huduma ya mionzi(ultraviolet (UV) light
DALILI ZA KANSA YA KWENYE UUME NI PAMOJA NA;
• Ngozi ya kwenye uume kuanza kubadilika rangi hasa ngozi ya mbele kwa wale ambao hawajatahiriwa
• Ngozi ya uume kuwa laini zaidi kuliko kawaida
• Ngozi ya uume kuanza kuwa na vipele pele au rashes, makovu au vidonda kwenye uume n.k
• Kuwa na uvimbe ambao unakuwa au kuongezeka ambao una rangi ya blue kwenda brown
• Ngozi ya uume kuanza kutoa harufu mbaya
• Kuwa na vidonda kwenye uume ambavyo wakati mwingine huvuja damu
• Uume kuvimba kwa mbele au kuwa na uvimbe chini ya ngozi ya uume
KUMBUKA; Uwepo wa dalili hizi haimaanishi moja kwa moja una kansa ya Uume,inawezekana pia ukawa na magojwa mengine kama magonjwa ya zinaa,maambukizi mbali mbali au tatizo la Allergy,hivo ukiona dalili kama hizi ongea na wataalam wa afya kwanza kwa ajili ya vipimo zaidi.
MATIBABU YA KANSA KWENYE UUME
Kama ilivyo aina zingine za kansa, Mgonjwa ambaye kagundulika mapema kuwa na tatizo hilo la kansa ya uume hupata tiba na kupona kwa haraka zaidi kuliko ukichelewa kugundulika na kuanza tiba mapema, matibabu huhusisha njia mbali mbali kama vile;
- Matumizi ya baadhi ya dawa mbali mbali ikiwemo cream za kupaka pamoja na vidonge vya kunywa
- Mwanaume kutahiriwa kwanza kama hakutahiriwa
- Huduma ya Cryotherapy n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!