TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

Tinnitus, Tatizo hili huhusisha mtu kusikia sauti za makelele au kitu kinaita(ringing) ndani ya sikio moja au yote mawili na sauti hizo hazitoki nje na wala hakuna mtu mwingine anazisikia zaidi ya mhusika mwenyewe.

Tatizo hili hutokea kwa watu wengi takribani asilimia 15% mpaka 20%, na hasa kwa watu wenye umri mkubwa au wazee, 

Mtu mwenye tatizo hili huweza kusikia sauti mbali mbali kati ya hizi hapa chini;

- Muito au ringing ndani ya sikio

Kubweka

- Kunguruma

- Kitu kinagonda ndani ya sikio

- sauti za Kusisimua au kutekenya N.k

CHANZO CHA TATIZO HILI LA TINNITUS

Hakuna sababu moja ambayo inasababisha tatizo hili,ila kuna mjumuisho wa sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili,na sababu hizo ni kama vile;

1. Tatizo la kupoteza usikivu,ambapo seli za vinyeleo ndani ya sikio kwenye sehemu ya ndani(Cochlea) ambazo zinasaidia sikio kupokea mawimbi ya Sauti kwa kupitia Auditory nerves kwenda kwenye ubongo,

Lakini baada ya ubongo kupokea hizo Electrical signals hutafsiri kama kelele badala ya sauti ya kawaida,na ndipo tatizo hutokea.

2. Nywele ndani ya sikio kupinda au kutoka zenyewe kutokana na sababu mbali mbali kama vile umri mkubwa au kuwa katika mazingira ambayo kunakuwa na sauti kubwa sana mara kwa mara kama vile ya muziki n.k, 

hali hii ya kuwa katika mazingira haya ya SAUTI KUBWA SANA inayopenya masikioni huweza kusababisha mtu kuwa na tatizo hili

3. Maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kwenye sikio kama vile bacteria,Fangasi,Virusi n.k

4. Tatizo la sikio kuziba kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuwa na maji mengi sikioni, nta kuzidi(EarWax), uchafu au kitu chochote ambacho kinaweza kuziba sikio lako

5. Kuumia kichwani au shingoni, hali hii huweza kuathiri sikio la ndani, nerves zinazosaidia sikio kusikia pamoja na utendaji kazi wa ubongo

6. Matumizi ya baadhi ya dawa, Mtu kuoverdose dawa au kutumia dawa kwa muda mrefu huweza kusababisha tatizo hili, na hapa tunazungumzia matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;

 dawa jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs(NSAIDs), Baadhi ya antibiotics, Dawa za kutibu kansa au saratani, Dawa jamii ya Diuretics, Antidepressants, Dawa za Malaria N.k

7. Matatizo ya muda mrefu yanayohusisha Nerves au mfumo wa Fahamu

8. Magonjwa kama vile Menieres ambayo huweza kusababisha abnormal Inner Ear fluid pressure n.k

9. Kutokufanya kazi vizuri kwa Eustachian tube ndani ya sikio

10. Tatizo kwenye mifupa ya sikio kama vile kukakamaa ndani ya sikio ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Otosclerosis

11. Tatizo la misuli yaani Muscle spasms ndani ya sikio

12. Matatizo kwenye mishipa ya damu ndani ya sikio ambayo huweza kuathiri mzuguko wa damu kwenye sikio, na matatizo hayo ni pamoja na; Atherosclerosis, Shinikizo la Damu(High blood pressure), Kinked, n.k

13. SABABU ZINGINE NI KAMA VILE;

- Ugonjwa wa kisukari

- Matatizo kwenye tezi la Thyroid

- Tatizo la maumivu makali sana ya kichwa cha mara kwa mara au Migraines

- Tatizo la Anemia au upungufu wa damu mwilini

- Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune disorders kama vile; Rheumatoid arthritis, Lupus n.k

MADHARA YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA

1. Mwili kuchoka kupita kiasi

2. Kupatwa na tatizo la mfadhaiko,msongo wa mawazo n.k

3. Kupata tatizo la kukosa usingizi

4. Kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu

5. Kushindwa kufanya kitu kimoja vizuri na kwa utulivu au kuloose concetration

6. Kuanza kupatwa na tatizo la wasiwasi kila mara

7. Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Matibabu ya tatizo hilo hutegemea na chanzo chake,hivo kwa ujumla zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile;

✓ Kuondoa nta au uchafu wowote ambao umeziba sikio

✓ Kutibu tatizo la mishipa ya damu,tatizo la presha,kisukari n.k

✓ Kuacha baadhi ya dawa au kubadilisha baadhi ya dawa

✓ Kupewa vifaa vya kukusaidia kusikia yaani Hearing aids n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Tatizo la Kelele Masikioni

1.Kukaa Sehemu Zenye Makelele mengi,

Kelele kubwa, kama vile zile za vifaa vizito,Vyuma kugongwa, misumeno ya minyororo na silaha za moto, ni vyanzo vikubwa vya upotezaji wa kusikia unaohusiana na kelele. 

Vifaa vya muziki vinavyotumia Sauti Kubwa Sana, vinaweza pia kusababisha upotevu wa kusikia unaohusiana na kelele kikichezwa kwa sauti kubwa kwa muda mrefu.  Watu wanaofanya kazi katika mazingira yenye kelele - kama vile wafanyikazi wa kiwanda na ujenzi, wanamuziki na wanajeshi - wako hatarini pia kupata tatizo hili la Kelele masikioni.

2. Umri

Unapozeeka, idadi ya nyuzi za neva zinazofanya kazi katika masikio yako hupungua, na hivyo kusababisha matatizo ya kusikia ambayo mara nyingi huhusishwa na tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.

3. Jinsia

Wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus kuliko wanawake.

4. Matumizi ya Pombe,na Tumbaku. 

Wavutaji sigara wana hatari kubwa ya kupata tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.  Kunywa pombe pia huongeza hatari ya kupata tatizo hili la masikio kupiga kelele tinnitus.

5. Baadhi ya Matatizo ya Kiafya.

 Hapa Nazungumzia matatizo mbali mbali ikiwemo;

  • Tatizo la Uzito mkubwa au Unene(Overweight/Obesity)
  • Matatizo ya Moyo(cardiovascular problems), 
  • Tatizo la Shinikizo la juu la Damu(high blood pressure)
  • Kuwa na historia ya kuumwa tatizo la arthritis 
  • Kuumia eneo la kichwani n.k

Jinsi ya Kuzuia Tatizo hili la Masikio kupiga Kelele au Masikio kunguruma

Katika hali nyingi, tatizo la Masikio kunguruma au masikio kupiga kelele(tinnitus) ni matokeo ya kitu ambacho hakiwezi kuzuiwa.  Hata hivyo, baadhi ya tahadhari zinaweza kusaidia kuzuia aina fulani za tinnitus;

Tumia vizuia kelele masikioni

 Baada ya muda, Makelele yatokanayo na sauti kubwa yanaweza kuharibu mishipa katika masikio, na kusababisha hasara ya kusikia na kupata tatizo la masikio kupiga kelele(tinnitus),

Hivo iwapo upo kwenye mazingira yenye kelele kubwa ambazo huwezi kuziepuka Jaribu kupunguza mawimbi makubwa ya sauti kwa kutumia vifaa vya kuzuia kelele masikioni.

 Na ikiwa huwezi kuepuka sauti kubwa, tumia kinga ya Masikio ili kulinda usikivu wako.  Ikiwa unatumia misumeno ya minyororo, ni mwanamuziki, unafanya kazi katika tasnia inayotumia mashine zenye sauti kubwa au kutumia bunduki (hasa bastola au bunduki), kila wakati vaa kinga ya kuzuia Sauti kubwa masikioni.

✓ Epuka mazingira yenye Sauti kubwa

Kama inawezekana kaa mbali na mazingira yenye Sauti kubwa,ikiwemo;

  • Mazingira yenye kelele kubwa za vifaa vya chuma,vyuma kugongwa
  • Misemo inayopiga kelele
  • Mashine za viwandani
  • Muziki mkubwa sana
  • Na aina zingine zote za Kelele kubwa

✓ Punguza sauti

Kukaa kwa muda mrefu kwenye mazingira ya kelele kubwa kama vile muziki mkubwa huweza kuathiri masikio yako na kusababisha tatizo la kelele masikioni,

Hivo kusikia sauti hizi bila ulinzi wa sikio au kusikiliza muziki kwa sauti ya juu sana kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani kunaweza kusababisha upotevu wa kusikia na tatizo la tinnitus.

Punguza Sauti kubwa ya Vifaa vya muziki Kama vile Earphone,Sabufa,Spika n.k

 ✓ Linda afya yako kwa Ujumla

Jikinge na matatizo mbali mbali ikiwemo;

  • Tatizo la Uzito mkubwa au Unene(Overweight/Obesity)
  • Matatizo ya Moyo(cardiovascular problems), 
  • Tatizo la Shinikizo la juu la Damu(high blood pressure)
  • Kuwa na historia ya kuumwa tatizo la arthritis 
  • Kuumia eneo la kichwani n.k

Fanya Mazoezi ya mara kwa mara, kula Mlo bora kiafya na kuchukua hatua nyingine ili kuweka mishipa yako ya damu kuwa na afya, Hii inaweza kusaidia kuzuia tatizo la tinnitus Linayohusishwa na fetma na matatizo ya mishipa ya damu.

✓ Acha kabsa au Punguza matumizi ya pombe, Sigara,Tumbaku au vitu vyenye kafeini nyingi na nikotini.

Vitu hivi zinapotumiwa kwa kiwango kikubwa, vinaweza kuathiri mtiririko wa damu na kuchangia kwenye tatizo la masikio kupiga kelele au tinnitus.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!