Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI (Acanthosis nigricans)



 NGOZI

• • • • •

TATIZO LA NGOZI YA KWAPA NA SHINGONI KUWA NYEUSI ZAIDI  (Acanthosis nigricans)


Tatizo la ngozi ya baadhi ya sehemu za mwili kuwa nyeusi zaidi ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama "Acanthosis nigricans" na tatizo hili hutokea sana kwenye maeneo ya SHINGONI,KWENYE KWAPA,NA SEHEMU ZA SIRI.


Mabadiliko haya ya rangi ya ngozi kwa asilimia kubwa huwapata watu wanene,wenye tatizo la kisukari, watoto wadogo ambao wapo kwenye hatari ya kuwa na kisukari yaani type 2 diabetes, na mara chache sana huweza kuwa kama dalili ya saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya ndani ya mwili kama vile ini,tumbo n.k


CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?


- Tatizo la acanthosis nigricans huweza kutokea baada ya Hormone au kichocheo cha INSULIN kushindwa kufanya kazi hali ambayo hupelekea pia kutokea tatizo la kisukari yaani type 2 diabetes.


- Matatizo kwenye vichocheo vya mwili(Hormone disorders) kama vile kichocheo kinachoipa ngozi rangi yake ya asili kuzidi sana yaani Melanini hyperpigmentation kwenye sehemu zilizoathirika na pia kwa watu wenye matatizo kama vile; tatizo la ovarian cysts, matatizo kwenye tezi la thyroid kama vile underactive thyroids au matatizo ya tezi la Adrenaline(adrenal glands).


- Matumizi ya baadhi ya dawa pamoja na virutubisho mfano; Mtu kutumia dose kubwa ya niacin, vidonge vya majira yaani birth control pills, dawa za prednisone pamoja na dawa zingine kama vile dawa jamii ya corticosteroids huweza kusababisha tatizo hili la acanthosis nigricans.


- Na pia kama nilovyosema hapo awali,mara chache sana tatizo hili huweza kuhusishwa na saratani au kansa ya viungo mbali mbali vya mwili kama vile Ini, Tumbo,utumbo n.k


KUMBUKA; Tatizo hili huwapata sana watu ambao;


• Ni wanene au wenye tatizo la uzito uliopita kiasi


• Wenye magonjwa kama kisukari


• Na wale ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wenye tatizo hili


MATIBABU YA TATIZO HILI LA ACANTHOSIS NIGRICANS


Tatizo hili huhisisha tiba za aina mbali mbali kulingana na chanzo chake,japo kwa ujumla kuna tiba kama vile;


✓ Kupunguza uzito wa mwili kama tatizo hili limetokana na mtu kuwa mnene au na uzito mkubwa


✓ Kuacha matumizi ya dawa ambazo huweza kusababisha tatizo hili


✓ Wengine hufanyiwa mpaka upasuaji ili kuondoa vivimbe au tumors kisha kusaidia ngozi ya mwili irudi kwenye rangi yake ya asili


✓ Lakini pia mtu huweza kutumia dawa mbali mbali kama vile;


   • Cream za kupaka kwenye ngozi


   • Baadhi ya sabuni za kuogea ambazo ni Antibacterial soaps


    • Dawa za kunywa yaani Oral acne medications N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments