Others
WHO yatangaza kifo cha mmoja wa wafanyakazi wake GAZA,Dima Abdullatif Mohammed Alhaj
Kwa majonzi mazito, WHO inatangaza kifo cha mmoja wa wafanyakazi wao huko Gaza, katika eneo linalokaliwa la Palestina.
Dima Abdullatif Mohammed Alhaj, mwenye umri wa miaka 29, amekuwa na WHO tangu Desemba 2019. Alifanya kazi kama msimamizi wa magonjwa katika Kituo cha viungo, “Limb Reconstruction Centre, a critical part of the WHO Trauma and Emergency Team”.
Dima alifariki wakati nyumba ya wazazi wake kusini mwa Gaza-ambako alikuwa amehamia kutoka Gaza City-ilipolipuliwa kwa bomu.
Aliuawa kwa kuhuzunisha pamoja na mume wake, mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miezi sita, na kaka zake wawili,
Inaripotiwa kuwa zaidi ya wanafamilia 50 na wanajamii waliokuwa wamejihifadhi katika nyumba moja pia walifariki.
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa