Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha: UNICEF
Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha: UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao.
Kwa msaada kutoka wakfu wa Bill na Melinda gates hivi karibuni UNICEF na shirika la afya duniani WHO nchini Tanzania walizindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo iliyowafikia watoto zaidi ya milioni 4.
Kutana na Therezia Kaminda muhudumu wa afya ya jamii miongoni mwa wahudu wengi walioshiriki kampeni hii chanjo ya nchi nzima mjini Sumbawanga mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania na anapita nyumba kwa nyumba kutoa chanjo hiyo,
“Kitu kinachonifurahisha kabisa ni uelewa walio nao wananchi wangu wameelewa vizuri na wameipokea chanjo hii kwa furaha”.
Kwa mujibu wa WHO kila ambukizi 1 kati ya 200 ya polio husababisha ugonjwa wa kupooza ambao hauwezi kubadilishwa na asilimia 5-10 miongoni mwa waliopooza hupoteza maisha. Pascal ni mzazi ameelimika kuhusu ugonjwa huu na amewapeleka mwanawe kupata chanjo sasa anataka elimu zaidi itolewe,
“Polio ni ugonjwa unaowapata watoto wa umri wa miaka 15 kushuka chini na una athari kubwa sana, kwa hiyo ni lazima watu waendelee kuelemishwa ili wawapeleke watoto ili wapatiwe chanjo. Watoto wangu wote chanjo walipata hata kuna wakati walitoa kwa watu wazima na hata chanjo ya Corona mimi nilipata”
Lengo la kampeni hii ya siku nne ni kumlinda kila mtoto na kwa Terezia uelewa kuhusu chanjo ni kitu cha msingi zaidi,
“Kabla ya hata ya kuwapa chanjo kwanza huwa nataka nifahamu wanafahamu nini kuhusu chanjo hii, lakini pia nawapa elimu kwa sababu siwezi kujua kama wote wameshapata tarifa au nini.”
Katika kampeni hiyo ya kuhakikisha kila mtoto anafikiwa na chanjo, watoto zaidi ya milioni 4.2 walipokea chanjo ya matone dhidi ya polio.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!