Connect with us

magonjwa

JINSI AMBAVYO MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUMLINDA MTOTO NA UMANJANO

Doctor Ombeni

Published

on

JINSI AMBAVYO MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUMLINDA MTOTO NA UMANJANO

Maziwa ya mama yanamchanganyiko wa virutubisho vingi vinavyoweza kupunguza tatizo la umanjano (Jaundice) kwa watoto wachanga.

Jaundice/unjano, ni tatizo linalosababishwa na mkusanyiko wa kiwango kikubwa cha bilirubini kwenye damu ya mtoto.

Bilirubini ni kati ya vitu vinavyo patikana ndani ya chembe hai nyekundu za damu (red blood cells-RBC) na ndizo zinazosababisha unjano wa ngozi kwa binadamu.

Kunapokuwa na uvunjikaji wa chembe nyekundu (RBC), bilirubini zinaachiwa kwenye mzunguko wa damu kisha zinapitishwa na kufanyiwa kazi kwenye maini (liver) na baada ya hapo zinatolewa mwilini.

Ila kwa baadhi ya watoto wachanga, maini yao yanakuwa hayajakomaa hivyo kukosa uwezo wa kuzibadilisha hizi bilirubin ili zitolewe nje ya mwili kiurahisi hivyo zinaishia kubaki katika mwili na kuleta hali ya unjano.

MUONEKANO WA MTOTO MWENYE UMANJANO

Maziwa ya mama yanaweza kupunguza unjano huu kwa njia zifuatazo:

  1. Kuupa mwili maji: asilimia kubwa (>80%) ya maziwa ya mama yametengenezwa na maji. Hivyo mtoto mchanga anapopewa maziwa ya mama kwa wingi inawezesha maini (liver) yake kufanya kazi vyema na kuweza kuziondoa hizi bilirubini kupitia njia ya mkojo na haja kubwa.
  2. Kolostramu (colostrum): Ni maziwa ya mama yale ya mwanzo ambayo ni mazito na yana rangi ya njano. Haya waziwa yanavirutubisho vinavyoweza kuupa mwili wa mtoto kinga juu ya magonjwa mbali mbali na pia yanaupa uwezo mwili wa kuvunja vunja na kuziondoa biliribun kwa kupitia njia ya mkojo na mfumo wa chakula.
  3. Mlo kamili: Maziwa ya mama yana virutubisho kamili vinavyowezesha ukuwaji mzuri wa mtoto. Mtoto anapopata virutubisho hivi kamili kwa njia ya maziwa, inawezesha mwili wa mtoto kuvunja vunja RBC kwa kiwango cha kawaida na kupelekea utengenezwaji mdogo wa bilirumini.
  4. Ulainishi wa choo: maziwa ya mama yanauwezo wa kulainisha choo na kuwezesha mtoto kupata choo vizuri. Kutokana na sababu hii, mtoto anaweza kutoa bilirubini mwilini na kupunguza nafasi ya kupata umanjano.
  5. Ngozi kuchukua mwangaza kiurahisi (light absorption): maziwa ya mama yana aina maalum ya kirutubisho (bilirumin isomer) chenye uwezo wa kunyonya (absorb) mwangaza unao tolewa wakati wa tiba ya umanjano na kupelekea urahisi wa kuvunja vunja bilirubini iliyo zidi mwilini.

Hitimisho:

Ni vyema kutambua umuhimu wa kumpa mtoto mchanga maziwa ya mama yake. Kwa kufanya hivyo tunamkinga mtoto juu ya magonjwa mbalimbali na kumwezesha awe katika nafasi ndogo ya kupata umanjano.

Cr: Dr.Kitange

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya wanawake14 hours ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital22 hours ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...

magonjwa ya watoto23 hours ago

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth)

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth) Maana ya mtoto njiti (Preterm Birth) Mtoto njiti ni mtoto anayezaliwa...

Afya News23 hours ago

Vifaa Tiba vya TSH.BILIONI 1.2 Kuimarisha huduma za dharura ya Uzazi na watoto wachanga

VIFAA TIBA VYA TSH.BILIONI 1.2 KUIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA YA UZAZI NA WATOTO WACHANGA Na Mvuda Jaffer, WAF – Arusha...

Afya News4 days ago

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO),...

Patient Stories5 days ago

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50...

Stars Health5 days ago

Joe biden aeleza hali yake ya saratani ya tezi dume kwa Sasa

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, ameeleza kuwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) unaendelea kuathiri shughuli zake...

Story5 days ago

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana Baadhi ya watu wanaweza kuishi vizuri kwa usingizi mfupi sana....

masikio5 days ago

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) ni yapi?

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) Masikio kupiga kelele ni tatizo la kiafya linalojulikana kitaalamu kama Tinnitus. Hali hii hutokea...

Utafiti7 days ago

Utafiti: Wanawake nchini Kenya wanazaa watoto wachache kadiri vifo vya wajawazito vinavyoendelea kuwa changamoto

Utafiti mpya wa afya ya uzazi nchini Kenya umeonesha kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja imeendelea kupungua, huku...