Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

Others

Kushambuliwa kwa hospitali na kukatwa kwa mawasiliano ni pigo kubwa kwa mfumo wa afya na raia Gaza: UN

Doctor Ombeni

Published

on

67 Views
0 Comments

Kushambuliwa kwa hospitali na kukatwa kwa mawasiliano ni pigo kubwa kwa mfumo wa afya na raia Gaza: UN

Watu wanaokimbia mapigano huko Gaza wanaendelea kutafuta maeneo salama ya kujihifadhi katika eneo hilo.

Hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbayĆ” katika Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati, huku hospitali zilizosalia zikiendelea kushambuliwa na kukatili maisha ya watu na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet vikizidisha adha yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Hali si hali Gaza maisha ya watu yanaendelea kupotea kila siku kwanza kutokana na mashambulizi lakini pia kwa kukosa huduma muhimu za afya kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye kupitia ukurasa wake wa X hii leo amesisitiza kwambaĀ ā€œMashambulizi dhidi ya hospitali , wahudumu wa afya na wagonjwa lazima yakome na usitishwaji mapigano ufanyike sasaā€

Dkt. Tedros pia amelaani vikali uharibifu mkubwa uliofanyika katika hospitali ya Kamal Adwan Kaskazini mwa Gaza baada ya kuvamiwa na vikosi vya Israel mwishoni mwa wikiĀ  ambapo wagonjwa wanane wameuawa akiwemo mtoto wa miaka 9.

Ameongeza kuwa wiki iliyopita vikosi vya Israel kwa siku nne viliivamia hospitali hiyo na kuipekua ndani nje huku kukiwa na taarifa za wahudumu wengi wa afya kushikiliwa.

Dkt. Tedros ameonya kwambaĀ ā€œMfumo wa afya wa Gaza ambao tayari ulikuwa taaban sasa kupoteza hospitali nyingine hata kama inafanya kazi kwa kiasi kidogo ni pigo kubwa kwa watu wa Gaza.ā€

Kivuko cha Shalom Karem (kutoka Maktaba)

Mahema ya watu waliofurushwa makwao yamesambaratishwa

Mkuu huyo wa WHO amesema wagonjwa wengi huko Kamal Adwan walilazimika kujiondoaĀ “katika hatari kubwa kwa afya na usalama wao”Ā huku magari ya kubeba wagonjwa yakishindwa kufika kituoni.

Ofisi yaUmoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dhariraĀ OCHAĀ imesema katika tarifa yake kwamba siku ya Jumamosi vikosi vya Israeli viliondoka hospitalini na kulingana na ripoti za vyombo vya habariĀ “buldoza la jeshi la Israeli lilisambaratisha mahema ya wakimbizi wa ndani nje ya hospitali, na kuua na kujeruhi idadi ambayo haijathibitishwa watuā€.

Tedros alisema kwenye mtandao wake wa X kwamba WHOĀ “inajali sana ustawi wa watu hao waliolazimika kukimbia makwao.ā€.

Kwa mujibu wa OCHA wizara ya afya ya Palestina mjini Ramallah imetaka uchunguzi ufanyike kuhusu tukio hilo.

OCHA pia ilinukuu jeshi la Israel likisema kuwa limewashikilia watu 90 kama sehemu ya operesheni hiyo naĀ “limepata silaha na risasi ndani ya hospitali”.

Kukatika kwa mawasiliano

Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa internet huko Gaza ambao ulianza Alhamisi iliyopita na kuendelea hadi mwishoni mwa wiki, OCHA imesisitiza katika tarifa yake ya hivi karibuni kwamba kuhusu hali ya kibinadamu katika Ukanda huo tarifa ni finyuĀ  kuanzia saa 24 zilizopita.

Huku shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesemaĀ ā€œGaza nzima sasa hakuna taarifa mpya zinazopatikana za vifo na majeruhi.ā€

Limeongeza kuwa katika Ukingo wa Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huu mpya Wapalestina 268 wameuawa na vikosi vya Israel wakiwemo watoto 70 ikiwa ni idadi kubwa Zaidi ya vifo vya Wapalestina kwa mwaka.

Shirika hilo limeonya kwamba kuendelesha kwa mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza kunasababisha ugumu mkubwa wa kuafikia wenye uhitaji na hivyo kuwafanya watu waendelee kuwa katikati ya vita, kuzingirwa na kukosa mahitaji.

OCHA imesema nako Gaza mamlaka ya afya ya Gaza haijasasisha idadi yao ya majeruhi tangu kuanza kwa kukatika kwa umeme, ambayo wakati huo ilikuwa imefikia vifo 18,787 na zaidi ya watu 50,000 kujeruhiwa tangu 7 Oktoba.

Kuendelea kwa mashambulizi ni hatari kubwa

Ofisi hiyo imeripoti kuendelea kwaĀ “mashambulizi mazito ya Israel katika Ukanda huo mwishoni mwa juma hasa huko Khan Younis kusini mwa Gaza na katika maeneo kadhaa ya mji wa Gaza kaskazini.ā€

Mapigano makali yalizuka kati ya wanajeshi wa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina huko Khan Younis na Rafah, pamoja na kuendelea kurusha makombora na makundi ya wapalestina yenye silaha nchini Israel, OCHA imesema.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotoĀ UNICEFĀ ambalo linasema ushitishwaji haraka wa mapigano wa muda mrefu kwa minajili ya kibinadamu ni lazimaĀ kwani sasa eneo zima la Gaza ambako Watoto walikuwa wakicheza na Kwenda shuleni kufurahia utoto wao limegeuka kifusi na kuwaacha njiapanda watoto hao.

Kivuko cha mpaka cha Kerem Shalom. (Maktaba)

Kivuko cha pili kimefunguliwa kwa msaada

Hali ya kibinaadamu katika eneo hilo bado ni mbaya kwani idadi kubwa ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao, wamesongamana katika eneo dogo kusini, wakikabiliwa na hali mbaya ya usafi na kukosa chakula na maji.

Umoja wa Mataifa unasema matumaini ya kuongezwa kwa misaada yameongezeka kutokana na tangazo la Ijumaa la kufunguliwa kwa kivuko cha mpaka cha Kerem Shalom kati ya Israel na Gaza, ambacho kulikaribishwa na jumuiya ya misaada.

Kivuko hicho kinaripotiwa kufunguliwa Jumapili kwa mara ya kwanza tangu tarehe 7 Oktoba.

Hadi wakati huu ni kivuko cha mpaka cha Rafah kusini pekee ndicho kilikuwa kimefunguliwa tangu usafirishaji wa misaada urejeshwe tarehe 21 Oktoba.

“Utekelezaji wa haraka wa makubaliano haya utaongeza mtiririko wa misaada,”Ā amesema mkuu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya dharura Martin Griffiths, na kuongeza kuwaĀ “lakini kile ambacho watu wa Gaza wanahitaji zaidi ni kumalizika kwa vita hivi”.

67 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

šŸ’¬ Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

šŸ†Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

WHO1 hour ago

Magonjwa ya Moyo yaendelea kuwa chanzo kikuu cha Vifo duniani

MAGONJWA YA MOYO YAENDELEA KUWA CHANZO KIKUU CHA VIFO DUNIANI Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu yanaendelea kuwa miongoni...

Afya News13 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS15 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips19 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume23 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO3 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa3 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital4 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

68
0