Madhara ya kumkalisha mtoto mapema
Mtoto kuanza kukalishwa mapema au kukaa mapema kabla ya wakati wake huweza kusababisha madhara mengi kiafya hasa kwenye mkao wa mwili hapo badae(Baby’s Body Posture),
Fahamu; Takriban asilimia 90% ya wazazi huwalazimisha watoto wao kuanza kukaa mapema kabla ya wakati,pasipo kujua madhara yake.
Ushauri; Acha Mtoto ajifunze mwenyewe kukaa, hakuna sababu ya kumharakisha kukaa. Watoto hufuata hatua za ukuaji wao wenyewe(Natural Gross Motor Development), na watafikia kipindi cha kukaa na kuanza kukaa wao wenyewe pasipo kulazimishwa
“Let your baby learn to sit on their own, there is no need to hurry or rush on. Babies will follow or reach their Natural Gross Motor Development on their own and without any hassles”.
Kuna wakati unaweza usione au kujua madhara ya mtoto kuanza kukaa mapema. Na kwa kutokujua huku, wazazi wakati mwingine huchukua hatua hizo ambazo zinachukuliwa kuwa si nzuri sana kwa watoto wachanga.
Wazazi wengi wanapenda kupiga picha za Watoto wao katika nguo na mitindo tofauti. Na wanapopiga picha huwaweka watoto wao wakiwa wameketi kwenye sofa au kochi wakiwa na tegemeo la mto kwa muda,
jambo ambalo linaweza kuwa sababu ya mtoto kukosa raha wakati na kipindi cha kupiga picha na hata wakati mwingine kuanza kupata maumivu ya mgongo.
Kuketi au kukaa kwa Mtoto hakuhitaji mchakato wowote wa kujifunza, Mkao utakuja wenyewe. Waache watoto peke yao wafurahie wakati wa kuanza kujizungusha kwa tumbo, kuzunguka, kutambaa, nk.
Madhara ya kumkalisha mtoto mapema
Wazazi wanaweza kuwa na nia Nzuri ya kutaka watoto wao wakae mapema, Lakini ukweli ni kwamba wanafanya kosa ambalo lina madhara kwenye ukuaji wa mtoto(Natural motor skills development).
Misuli ya Mtoto bado inakuwa kwenye mchakato wa kutanuka na kujiimarisha, lakini kuilazimisha kufanya hivo utaifanya kuwa dhaifu zaidi,
Madhara ya Mtoto kukaa mapema kabla ya wakati wake ni pamoja na;
1. Kupata tatizo la maumivu ya mgongo,
Kumkalisha mtoto wako mapema au kumlazimisha mtoto kukaa kabla ya wakati wake unaweza kusababisha tatizo la maumivu ya mgongo hapo badaee kwenye maisha yake,
Madhara ya mgongo huweza kutokea hasa kutokana na mifupa ya mgongoni kuwa dhaifu sana (low strength of the backbone).
2. Viungo kuwa dhaifu ikiwemo miguu,mikono,mabega pamoja na mgongo.
Madhara ya mtoto kuanza kukalishwa mapema kabla ya wakati wake ni pamoja na; kudhoofika kwa viungo muhimu vya mwili kama vile;
- miguu,
- mikono,
- mabega
- pamoja na mgongo
Na matokeo yake husababisha hatua zingine za ukuaji kuchelewa, mfano; hatua ya kutambaa,kutembea n.k
3. Kuathiri Mkao wa mwili kwa mtoto(Baby’s Body Posture), Movements & Body Stability.
Kuanza mtoto kukalishwa mapema itaathiri vitu vyote hivi kwa mtoto wako.
Epuka tabia ya kumlazimishia mtoto wako kukaa, acha ajifunze mwenyewe….,!!!!
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!