Others
Hospitali za rufaa zote nchini zijengwe kwa kufuata ‘master plan’
Hospitali za rufaa zote nchini zijengwe kwa kufuata ‘master plan’
Na. WAF – Arusha
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini kujengwa miundombinu yake kwa kufuata ‘master plan’ na kuacha kujenga majengo madogo ya chini kama vibanda ili kupunguza gharama za uendeshaji kwa Serikali na usumbufu kwa wagonjwa.
Waziri Mhe. Ummy Mwaalimu amesema hayo leo Disemba 30, 2023 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha baada ya kufanya ziara katika Hospitali hiyo.
“Nimesikiliza maono yenu na matarajio yenu mnataka kuanzisha maswala ya Kemotherapi, jengo la OPD sasa kabla hamjaendelea nataka mzingatie ‘master plan’ ya mejengo ya Hospitali.” Amesema Waziri Ummy
Amesema, ifike wakati tuachane na mambo ya vibanda vibanda kila sehemu, siku hizi unaweza ukawa na jengo moja tu ambalo huduma zote zinapatikana katika jengo hilo ili kupunguza kharama za umeme, maji pamoja na gharama nyingine za uendeshaji.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaAidha, Waziri Ummy amesisitiza matumizi ya Telemedicine kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi na kuwajengea uwezo wataalamu wengine katika ngazi ya Wilaya pamoja na vituo vya Afya ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Pia, Waziri Ummy ameahidi kuwapelekea Kipashajoto cha mtoto (Baby Warmers) 11 katika Hospitali hiyo ya Mount Meru angalau vifike 14 kwa ajili ya kuokoa watoto wachanga wanaopata changamoto za kiafya.
“Mhe. Rais ameshaelekeza anataka huduma bora za Afya zitolewe kwa Watanzani kwa kuwa ameshatoa fedha kwa ajili ya vifaa pamoja na dawa hivyo ni jukumu letu sisi wasimamizi na watendaji kutoa huduma bora za Afya.” Amesema Waziri Ummy.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)