Mpaka Sasa Mikoa Sita ya Tanzania ina kipindupindu.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023 katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema mpaka sasa kuna Mikoa sita ambayo inaendelea na mlipuko wa kipindupindu nchini.
Waziri Ummy amenukuliwa akisema “kwa mwaka jana 2023 mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulitolewa taarifa katoka Mikoa 12 nchini ambapo Wagonjwa 927 na vifo 27 vilitolewa taarifa, Mkoa wa Arusha uliongoza kwa visa 214 lakini bahati nzuri hakukutokea kifo, katika Mkoa wa Mara jumla ya visa 193 na vifo vinane (8) vilitolewa taarifa, Mkoa wa Simiyu Visa 184 na vifo Viwili (2)”
“Mpaka sasa kuna Mikoa 6 ambayo inaendelea na mlipuko ambayo ni Shinyanga, Ruvuma, Tabora, Simiyu, Mwanza na Kagera”
Waziri Ummy amewapongeza Wakuu wa Mikoa pamoja na watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri kwa kuendelea kuimarisha usimamizi ili ugonjwa huo udhibitiwe.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!