Njia za uzazi wa mpango kwa mama anayenyonyesha
Baada ya mama kujifungua moja ya vitu ambavyo hukutana navyo mwanzoni ni swala la kupanga Uzazi, ili kuzaa watoto kwenye mpangilio unaoeleweka.
Kuna dhana nyingi kuhusu uwezo wa kubeba Mimba baada ya kujifungua, ukweli ni kwamba, baada ya mzunguko wako wa hedhi kurudi mahali pake na yai kuanza kutoka kwenye ovary(Ovulation) unaweza kubeba mimba tena hata kama hujaona period yako,
Kwani period ni matokeo ya yai kutokurutubishwa, hivo hutolewa nje kama uchafu.
Fahamu: Unyonyeshaji hupunguza uwezekano wa mama kubeba mimba, ingawa lazima uwe ule unyonyeshaji sahihi(exclusively breastfeeding).
Na njia hii huweza kufanya kazi kwa miezi sita ya mwanzo pekee baada ya mtoto kuzaliwa.
Ili Unyonyeshaji uwe kinga dhidi ya Ujauzito, lazima umnyonyeshe Mtoto wako angalau kwa kila baada ya masaa manne wakati wa mchana na angalau masaa sita wakati wa usiku, bila kumpa kitu kingine chochote isipokuwa maziwa yako tu.
Fahamu ni Lazima yai litoke kwanza(ovulation) ndipo upate hedhi yako ya kwanza baada ya kujifungua kama sio mjamzito,
Sasa kwa vile hujui yai litatoka lini(ovulate) hivo upo kwenye hatari ya kubeba mimba tena usipochukua tahadhari na kujikinga.
Na Njia hii ya Unyonyeshaji haiwezi kufanya kazi vizuri ikiwa tayari period yako ilisharudi(tayari umeshaanza kuona siku Zako za hedhi) This method isn’t effective if your period has already returned.
Hivo basi, ikiwa unahitaji kutumia njia hii lazima upewe maelekezo ya kutosha na uelewe kabla ya kuanza kuitumia kwani hatari ya kupata Ujauzito huweza kuwa kubwa Zaidi.
Njia za uzazi wa mpango kwa mama anayenyonyesha
Njia Zingine za Uzazi wa mpango kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na;
– Kitanzi(IUD);
Kitanzi au Intrauterine devices (IUDs) ni njia yenye ufanisi wa zaidi ya asilimia 99% kwenye kuzuia mimba na inaruhusiwa hata wakati unanyonyesha.
Kuna IUDs za aina mbili;
- kuna zenye vichocheo ndani yake(hormonal IUDs)
- Kuna ambazo hazina(Non-hormal IUDs)
– Vidonge vya Uzazi wa mpango(Mini-pill);
Hapa kuna angalizo, vidonge vya uzazi wa mpango vipo vya aina mbili, kuna vile vya rangi mbili na vile vya rangi Moja,
Vile vya rangi mbili(combined oral contraceptives pills) vina mchanganyiko wa vichocheo vya aina mbili estrogen na progestin ambapo huathiri uzalishwaji wa maziwa, Hivo usitumie vidonge vya aina hii wakati unanyonyesha.
Tumia vile vya rangi Moja(Mini-Pill) ambavyo vina kichocheo cha aina moja ambacho ni progestin kama umeamua kutumia vidonge.
– Matumizi ya Condoms
Njia nyingine ya Uzazi wa mpango ambayo huruhusiwa wakati unanyonyesha ni Condoms,
Zipo condom za kiume na zipo condom za kike, Hivo ni uamuzi wenu nani avae Condom kati yenu.
– Matumizi ya Kijiti(Implant);
Vijiti vipo vya aina mbili, kuna cha miaka 3 pamoja na kile cha Miaka 5, Hivo inategemea na wewe unataka kupanga Uzazi wa aina gani.
Ila njia hii pia inaruhusiwa kutumia hata wakati unanyonyesha.
– Matumizi ya Sindano(Depo-Provera shot);
Wapo pia wanaotumia Sindano(Depo-Provera) ili kujikinga na mimba, na hii ni Inatumia homoni ya progestini kuzuia mimba,
Uchomaji wa Sindano hukupa ulinzi wa miezi mitatu pekee kwa wakati mmoja, kwa hivyo utahitaji kufuatilia kila baada ya miezi mitatu, Maana baada ya miezi3 hutakuwa na kinga tena, hivo utatakiwa kupata nyingine.
– Njia za asili(Natural family planning);
Njia hizi hazihusishi vichocheo vyovyote ila zinahitaji uelewa mkubwa,umakini na kufuata maelekezo sahihi ili kujikinga na Mimba.
Hapa tunazungumzia njia kama vile matumizi ya kalenda n.k
– Kuvunga Uzazi kabsa(Sterilization);
Ikiwa huhitaji kubeba Mimba tena kwenye maisha yako,
Njia itakayofuata ni kufunga kabsa Uzazi, ambapo inajulikana kama Female sterilization au kwa majina mengine kama vile; tubal sterilization, tubal ligation, au “getting your tubes tied.”
Ni matumaini yangu kuwa Umepata elimu kuhusu Njia Za Uzazi wa Mpango zinazoruhusiwa wakati unanyonyesha.
Bonus Tips:
Mimi,Njia ambayo naipendekeza Kwako kuitumia wakati unanyonyesha ni – Kitanzi(IUD);
Kuna IUDs za aina mbili;
- kuna zenye vichocheo ndani yake(hormonal IUDs)
- Kuna ambazo hazina(Non-hormal IUDs)
Nakushauri utumie ambazo hazina vichocheo ndani yake(Non-hormal IUDs/Copper).
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!