Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF. JANABI: wekeni utaratibu wa kuandika wosia



PROF. JANABI: wekeni utaratibu wa kuandika wosia.

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amewashauri watumishi wa hospitali hiyo kuwa na utaratibu wa kuandika wosia kwa lengo la kupunguza changamoto mbalimbali pale itakapotokea watumishi hao wamepoteza maisha.

Prof. Janabi ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kinachoendelea Jijini Dar es Salaam ambapo kimewakutanisha watumishi wa Upanga na Mloganzila.

Prof. Janabi ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na migogoro miongoni mwa ndugu na wanafamilia wa mtumishi husika na kuongeza kuwa endapo mtumishi ataandika wosia migogoro haitajitokeza kwakuwa mpangilio na magawanyoa wa mali zake utakuwa umeanishwa katika wosia.

“Wosia unaweza kuandaliwa wakati wowote na jukumu linalobaki ni kuhuisha wosia huo kulingana na mabadiliko yanayotokea ikiwemo ongezeko la idadi ya watoto na mali anazozimiliki mhusika” Amesema Prof. Janabi

Pia,amesisitiza kuwa wosia unasaidia mtumishi kutopoteza mali zake kwakuwa zote zitakuwa zimeandikwa na mgawanyo wake umewekwa wazi hivyo hakuna mtu au kikundi kinachoweza kuidhulumu familia.

Wosia ni tamko lenye nguvu kisheria linalotolewa na mtu kwa hiyari ili kuonesha namna gani mali zake zitagawanywa kwa lengo la kuondoa au kuizuia migogoro inayoweza kujitokeza juu ya mali za mtoa wosia pindi atakapofariki.



Post a Comment

0 Comments