Ugonjwa wa trichomoniasis,chanzo,dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa trichomoniasis,chanzo,dalili na Tiba yake

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA TRIKOMONASI,CHANZO,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Trichomoniasis ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa, Tatizo hili mtu huweza kulipata kwa njia ya kujamiiana.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA Trichomoniasis

Ugonjwa huu wa Trikomonasi hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS.

Dalili za Ugonjwa wa trichomoniasis

DALILI ZA UGONJWA WA TRIKOMONASI NI PAMOJA NA;

(a) Kwa Wanawake

1. Mgonjwa kupata miwasho sehemu za siri ambapo hupata miwasho maeneo ya kuzunguka ukeni ikiwemo pamoja na ngozi ya mashavu ya uke.

2. Kutokwa na uchafu sehemu za siri  wenye rangi kama njano,nyeupe au Kijani kwa mwanamke

3. Mwanamke kuvuja damu sehemu za siri

4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu pamoja na kuvimba

5. Kuhisi hali kama ya kuungua sehemu za siri mara kwa mara

6. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

7.Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa

8. Kupata hisia za mkojo mara kwa mara ndani ya mda mfupi

(b). Kwa Wanaume

1. Mgonjwa kupata miwasho sana sehemu za siri, kwenye Njia ya Mkojo ikiwemo eneo la kitundu kidogo cha mkojo kwenye uume

2. Kutokwa na uchafu kwenye Njia ya mkojo

3. Kuhisi hali ya kuchomwa au kuungua baada ya mwanaume kutoa mbegu za kiume au baada ya mwanaume kumwaga shahawa akifanya mapenzi

4. Kuhisi hali ya kuungua au kuchomwa wakati wa kukojoa

5. Kupata hisia za kukojoa mara kwa mara ndani ya mda mfupi

Kundi lililopo kwenye hatari ya Kupata Ugonjwa wa trichomoniasis

WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YAKUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;

1. Watu wenye wapenzi wengi

2. Watu ambao wameshawahi kupata tatizo hili hapo nyuma

3. Watu ambao wanashiriki mapenzi bila kinga au wanaofanya ngono zembe

4. Watu wenye historia ya kupata magonjwa mengine ya zinaa kama kaswende au kisonono

MATIBABU YA Ugonjwa wa trichomoniasis

Ugonjwa huu hutibika na moja ya matibabu makubwa ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics. Mgonjwa huweza kupewa dawa aina ya Tinidazole pamoja na Metronidazole hilo tatizo likaisha kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!