Connect with us

Others

WHO yazindua ombi la dola bilioni 1.5 kwa ajili ya dharura kwa 2024

Doctor Ombeni

Published

on

51 Views
0 Comments

WHO yazindua ombi la dola bilioni 1.5 kwa ajili ya dharura kwa 2024

Mwanamke akipokea matibabu katika kituo cha matibabu ya kipindupindu nchini Sudan(Picha)

Shirika la Afya Duniani WHO leo limezindua ombi la dola bilioni 1.5 kulinda afya ya watu walio hatarini zaidi katika dharura 41 kote ulimwenguni kwa mwaka 2024.

Ombi hilo linahusu dharura zinazodai kiwango cha juu zaidi cha hatua za kuzikabili nazo kutoka kwa WHO, kwa lengo la kufikia zaidi ya watu milioni 87. Ombi hilo limetolewa katika muktadha wa dharura tatakuanzia migogoro, mabadiliko ya tabianchi na kuyumba kwa uchumi, ambazo zinaendelea kuchochea watu kuhama na kukimbia makwao, njaa na ukosefu wa usawa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus

“Kwa wale wanaokabiliwa na dharura, kukatizwa kwa huduma muhimu za afya mara nyingi kunamaanisha tofauti kati ya maisha na kifo. Kuanzia akina mama wanaojifungua wakati wa migogoro, misaada kwa watoto wadogo katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame, kwa wale wanaopata matibabu ya saratani au dialysis, huduma za afya huokoa maisha. Na huduma za afya pia ni muhimu kwa kuvunja mzunguko ambao mara nyingi huacha jamii katika hali ya hatari na kutegemea msaada zaidi wa dharura,” 

Msaada huo wa fedha utaokoa maisha

WHO inasema msaada huo kwa mwaka 2024 utawezesha huduma ya afya ya kuokoa maisha, usambazaji wa vifaa muhimu vya afya na vinginevyo, pamoja na ukarabati wa huduma muhimu za afya ili kuhakikisha huduma endelevu.

Limeongeza kuwa ufadhili huo unasaidia upatikanaji wa moja kwa moja wa huduma za afya kwa jamii katika maeneo ambayo ni magumu kufikiwa, kwa ushirikiano na mashirika ya ndani na hatua madhubuti za kufuatilia, kushiriki habari na kuandika kuhusu milipuko na mashambulizi kwa wahudumu wa afya. Vitendo vingine muhimu ni kudumisha mifumo iliyopo ya utunzaji wa afya na kujenga mnepo dhidi ya vitisho vya siku zijazo.

Ombi hilo linabainisha thamani chanya ya ufadhili kusaidia watu wenye mahitaji ya kibinadamu.

Kila dola moja ya Marekani iliyowekezwa katika WHO inatoa faida kwa uwekezaji wa angalau  dola 35.

Mgawanyo wa fecha za msaada huo kikanda

Ufadhili huo utakwenda katika kanda mbalimbali za WHO ambapo Kanda ya Afrik itapata dola milioni 334, Kanda ya Mediterania ya Mashariki itapokea dola milioni 705, kanda ya Ulaya dola milioni 183, Kanda ya Pasifiki ya Magharibi dola milioni 15.2, Kanda ya Kusini-Mashariki ya Asia dola milioni 49 na Kanda ya Amerika dola milioni 131.

Dk Tedros amesema “Kwa msaada wa wafadhili, tutaokoa maisha, kukidhi mahitaji muhimu ya afya kwa walio hatarini zaidi, na kusaidia jamii kujikwamua kutoka kwa majanga na kuwajengea uwezo mkubwa wa kukabiliana na matishio ya kiafya siku zijazo. “

Ameendelea kusema kwamba “WHO inathamini usaidizi wote uliopokelewa mmwaka 2023, ambao ulituruhusu kusaidia mamilioni ya watu. Tunapoingia 2024, mshikamano na uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa unahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.”

51 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

52
0