Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa kipindupindu
Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa kipindupindu.
Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo zitakazosaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu uliolilikumba taifa hilo la Kusini mwa Afrika tangu mwezi Oktoba mwaka jana.
Umoja wa Mataifa umeidhinisha hizo. Kulingana na data za hivi karibuni zilizotolewa na wizara ya afya mjini Lusaka, mpaka sasa zaidi ya watu 365 wamekufa kutokana na ugonjwa huo na watu 418 wameambukizwa ugonjwa huo.
Muda wa kufunguliwa shule na vyuo umesogezwa mbele kutoka tarehe 8 Januari hadi tarehe 29 wakati serikali ikiendelea na juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!