chanzo cha kukosa choo
Dalili za kukosa choo,chanzo chake na Tiba
Dalili za kukosa choo,chanzo chake na Tiba
Ikiwa mtu hajapata Choo kwa wiki nzima, lakini anahisi vizuri, anapaswa kutafuta ushauri wa matibabu hata kama anajiona yupo Sawa.
Na upande wa kupata Choo ni Mara ngapi kwa Siku ambapo ni Sawa kiafya tazama hapa.Muda Sahihi wa kupata Choo kwa Siku.
Kwa wengine, kukosa Choo mara kwa mara hutokana na mabadiliko machache ya mtindo wa maisha au mabadiliko ya lishe, au kwa kutumia baadhi ya dawa.Watu wenye tatizo la kukosa choo kupita kiasi wanaweza kuhitaji matibabu.
Dalili za kukosa choo
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za tatizo la Kukosa Choo unazoweza kuzipata;
1. Kupata choo chini ya mara tatu(3) kwa muda wa wiki nzima
2. Wakati ukijisaidia kinyesi kinakua kigumu na kimekauka
3. Unapata shida sana ya kujisaidia au unapata maumivu sehemu ya haja kubwa hata wakati choo kinatoka
4. Unapata maumivu ya tumbo au tumbo kukaza
5. Unahisi tumbo kujaa lakini ukijisaidia hamna kitu
6. Kuhisi hali ya kichefuchefu mara kwa mara
7. Baada ya Kujisaidia lakini bado unahisi kuna kitu kimebaki ndani(kama bado hujajisaidia ukamaliza) n.k
Ikiwa unakosa Choo lakini pia unapata dalili hizi hakikisha unawahi kwenye matibabu au kwa Ushauri Zaidi tuwasiliane ndani ya @afyaclass;
- Unapata Maumivu makali sana ya Tumbo
- Tumbo kuvimba
- Unahisi kichefuchefu na kutapika
- Unapata Homa
- Unapata Maumivu makali ya Mgongo
- Unajisaidia Damu n.k
Chanzo cha kukosa choo
Kuna Sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia tatizo la kukosa Choo ikiwemo;
– Kutokula vyakula vyenye nyuzi nyuzi(fibers) za kutosha
– Kutokunywa maji ya kutosha au kuwa na tatizo la Upungufu wa maji mwilini
– Kutokufanya Mazoezi ya mwili
– Kubadilisha mazingira na kwenda Sehemu ya Ugenini
– Kutumia kwa kiwango kikubwa sana Maziwa au bidhaa za maziwa
– Kuwa na Msongo wa Mawazo
– Matumizi ya baadhi ya dawa, Mfano wa dawa hizo ni kama vile;
- Dawa jamii ya Strong pain medicines, kama zile zenye narcotics mfano;codeine, oxycodone (Oxycontin®) na hydromorphone (Dilaudid®).
- Dawa jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), kama vile ibuprofen (Advil®, Motrin®) na naproxen (Aleve®).
- Dawa jamii ya Antidepressants, kama vile selective serotonin reuptake inhibitors (mfano fluoxetine [Prozac®]) au tricyclic antidepressants (mfano amitriptyline [Elavil®]).
- Dawa jamii ya Antacids zenye calcium au aluminum, mfano Tums®.
- Dawa jamii ya Iron pills.
- Dawa za mzio(Allergy medications), kama antihistamines (mfano diphenhydramine [Benadryl®]).
- Baadhi ya dawa za shinikizo la dami kama zile zenye calcium channel blockers (mfano verapamil [Calan SR®], diltiazem [Cardizem®] na nifedipine [Procardia®]) pamoja na beta-blockers (mfano atenolol [Tenormin®]).
- Dawa jamii ya Psychiatric medications, mfano clozapine (Clozaril®) na olanzapine (Zyprexa®).
- Dawa jamii ya Antiseizure medications, kama vile phenytoin na gabapentin.
- Dawa jamii ya Antinausea medications, kama vile ondansetron (Zofran®).n.k
– Kuwa na baadhi ya Matatizo ya kiafya(Medical conditions) kama vile;
- Matatizo ya tezi la thyroid kutokufanya kazi vizuri-underactive thyroid gland (hypothyroidism),
- Ugonjwa wa Kisukari
- Tatizo la uremia pamoja na hypercalcemia.
- Kuwa na Saratani kama vile ya Utumbo mpana(Colorectal cancer).
- Kuwa na tatizo la Irritable bowel syndrome (IBS)
- Tatizo la Diverticulitis.
- Obstructed defecation syndrome
- Tatizo la Intestinal pseudo-obstruction.n.k
– Kuwa na matatizo kwenye mfumo wa Nerves(Neurologic disorders) ikiwemo;
- Tatizo la kuumia uti wa mgongo(spinal cord injury)
- Tatizo la multiple sclerosis,
- Ugonjwa wa Parkinson’s disease
- Pamoja na stroke.
Ikiwa una tatizo hili la kukosa Choo hakikisha unapata Msaada wa matibabu pamoja na Vitu vya Kufanya na kuzingatia.
NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
chanzo cha kukosa choo
Tatizo La Kukosa Choo Chanzo Na Tiba yake
Tatizo La Kukosa Choo Chanzo Na Tiba yake
Tatizo la kukosa choo ni hali ambayo mtu anapata ugumu wa kujisaidia au hapati haja kubwa kwa siku kadhaa (mara nyingi chini ya mara 3 kwa wiki). Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kulingana na chanzo chake.
Kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation) ni tatizo linalotokea kwa Watu wengi, na baadhi ya Tafiti huonyesha kwamba huathiri karibu 20% ya watu kila mwaka (Cirino, 2019).
Na hapa ndani ya afyaclass tunapata Si chini ya wagonjwa 5 kwa Siku,kila Siku wenye changamoto ya aina hii, kwa kuliona tatizo hili jinsi ambavyo huendelea kusumbua watu wengi,tumeona umuhimu mkubwa wa kukuelimisha wewe.
Kama wewe ni Miongoni mwa Watu wenye Shida hii,Unahitaji kujua Sababu zake na nini cha kufanya ili uondokane na hali hii.
Tuangalie Sababu mbali mbali za Tatizo hili la kukosa Choo katika Makala Hii,,
Chanzo cha Tatizo la Kukosa Choo
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kukosa choo na Sababu Hizi ni pamoja na:
1. Kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi(fibers ndogo)
Baadhi ya Watu huweza kupata tatizo la kukosa choo kwa Sababu hawali vyakula vyenye nyuzinyuzi(fibers) za kutosha.
Tafiti nyingi huonyesha Kula vyakula vya nyuzinyuzi zaidi kunaweza kusaidia kupunguza au kuondoa tatizo hili la Kukosa Choo.
Mifano ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa makundi ambavyo hupatikana kwenye jamii zetu ni pamoja na:
-Mboga za majani kama vile:
- Sukuma wiki
- Spinachi
- Mchicha
- Kabeji
- Ulaji wa Karoti n.k.
– Kula Matunda kama vile;
- Papai
- Tufaha (apple)
- Ndizi (hasa mbivu za kijani kidogo)
- Embe
- Tikiti maji
- Chungwa n.k
– Vyakula vya nafaka kama vile;
- Unga wa dona
- Ngano nzima
- Mahindi yasiyokobolewa
– Maharage na jamii zake
- Maharage ya kawaida
- Kunde
- Njugu
- Choroko
- Dengu
– Mbegu na karanga
- Mbegu za maboga
- Mbegu za alizeti
- Karanga n.k.
Fahamu kwamba; Kula vyakula vingi vya wanga vilivyosindikwa kama mikate meupe, wali mweupe, au viazi bila mboga huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo hili.
2. Kutokunywa maji ya kutosha
Upungufu wa maji mwilini hufanya kinyesi kuwa kigumu na kigandamane, Lakini pia hukuweka kwenye hatari zaidi ya kukosa choo kabsa.
3. Matumizi ya baadhi ya Dawa
Baadhi ya dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za maumivu au jamii ya opioids, baadhi ya dawa za Presha,Dawa za madini chuma n.k. zinaweza kupunguza usagaji chakula na kusababisha tatizo la kukosa choo.
Pia dawa jamii ya Antidepressants,Baadhi ya Antacids,antihistamines n.k..
4. Kuziba kwa njia ya haja kubwa
Tatizo hili pia linaweza kusababisha Mtu asipate choo kabsa.
5. Uwepo wa Magonjwa mbali mbali
Magonjwa kama vile Kisukari, matatizo ya tezi kama vile tatizo la hypothyroidism, ugonjwa wa koloni au utumbo mpana au Irritable bowel syndrome (IBS), au kuwa na saratani ya utumbo,Vyote hivi huweza kuchangia tatizo la kukosa choo.
Fahamu kwamba matatizo yote yanayosababisha Uharibifu wa neva mbalimbali katika njia ya usagaji chakula yanaweza kupunguza usagaji chakula, na kusababisha dalili hizi za kukosa choo kwa mgonjwa.
Majeraha ya neva, kama vile kwenye eneo la uti wa mgongo au majeraha ya ubongo, yanaweza pia kupunguza usagaji chakula, na kupelekea tatizo hili la kukosa choo kabsa.
6. Sababu zingine za kawaida ni pamoja na;
- Kukosa mazoezi
Mwili usiotembea au kufanya shughuli au mazoezi huchangia utumbo kufanya kazi taratibu, na hii huweza kuongeza hali hii ya kukosa choo
- Kuchelewesha haja kubwa mara kwa mara
Mtu akizoea kuzuia haja kubwa, misuli ya utumbo hupoteza msukumo wa kawaida, na huweza kuwa kwenye hatari ya kukosa choo pia.
- Mabadiliko ya Kimaisha
Kuwa na Msongo wa mawazo, ujauzito, au safari ndefu zinaweza kubadilisha mpangilio wa choo.
Zingatia Mambo haya Muhimu sana kwako
1. Fanya Mabadiliko ya lishe yako,Ongeza vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile:
Mboga za majani kama (sukuma, mchicha, kabichi)
Matunda (papai, embe, parachichi, ndizi mbivu)
Nafaka zisizosindikwa (mtama, ulezi, unga wa dona)
Epuka vyakula vya kukaanga sana na vyakula vya mafuta mengi.
2. Kunywa maji ya kutosha
Angalau glasi 6–8 za maji kila siku.
Maji ya uvuguvugu asubuhi yanaweza kusaidia kusisimua utumbo.
3. Fanya Mazoezi ya mwili
Kutembea kwa dakika 30 kila siku husaidia kuamsha utumbo na kuondoa hali hii ya kukosa choo.
4. Kuanzisha ratiba ya kwenda chooni
Jisaidie kila siku muda uleule, hasa baada ya kula.
5. Tiba ya dawa (ikiwa njia asili hazijasaidia)
Pata Dawa za kuondoa tatizo hili,Tumia dawa kwa ushauri wa daktari tu, kwani matumizi mabaya yanaweza kusababisha madhara zaidi.
Je,Una tatizo hili na hujapata Msaada wa Tiba?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Rejea Sources:
- https://www.medicalnewstoday.com/articles/327136#causes
- https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/4059-constipation
- https://cdhf.ca/en/constipation-what-to-do-if-you-cant-poop/#:~:text=Constipation%20is%20quite%20common%2C%20affecting,can%20indicate%20something%20is%20wrong.
-
magonjwa2 years ago
Muwasho sehemu za siri kwa mwanaume chanzo chake
-
afya5 years agoCHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu2 weeks ago
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu au maji ya uzazi
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu2 weeks ago
Madhara ya Mtoto Kunywa Maji Machafu: Dalili, Hatari na Namna ya Kumsaidia
-
Madhara ya Pombe1 week agoJE, POMBE hupunguza testosterone na Ubora wa mbegu za Kiume?
-
afya5 years agoDawa za Kukausha kidonda,kuzuia maambukizi Na SABABU za Kidonda Kutokupona Haraka
-
Afya News1 week agoDaktari amfanyia Upasuaji Mama kumtoa Mtoto ili kumfanyia upasuaji wa Uvimbe Kisha Kumrudisha tena tumboni
-
choo chenye makamasi1 week ago
Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha


.jpeg)
.jpeg)


