Ticker

6/recent/ticker-posts

Gwiji wa Kombe la Dunia la Ujerumani Andreas Brehme, 63, afariki kutokana na mshtuko wa moyo



Gwiji wa Kombe la Dunia la Ujerumani Andreas Brehme, 63, afariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Gwiji wa Kombe la Dunia la Ujerumani, Andreas Brehme, ambaye aliifungia Ujerumani Magharibi bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia 1990, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.

Gazeti la Ujerumani la Bild liliripoti kwamba Brehme alifariki Jumatatu usiku, Febuari 19, mjini Munich, kwa mshtuko wa moyo(cardiac arrest).

Inasemekana kwamba Brehme alilazwa katika chumba cha dharura cha kliniki ya Ziemssenstrasse, karibu na nyumba yake, lakini hakuweza kuokolewa.

Brehme aliichezea Ujerumani mara 86 wakati wa uchezaji wake na Kaiserslautern, Bayern Munich, na Inter Milan miongoni mwa nyingine katika ngazi ya klabu.

Beki huyo wa kushoto alifunga mkwaju wa penalti dakika ya 85 huku vijana wa Franz Beckenbauer wakiilaza Argentina 1-0 mjini Rome.

Uchezaji wa kimataifa wa muongo wa Brehme, ambao ulikuwa na mabao manane, ulimshuhudia akicheza kwenye Kombe la Dunia la 1986, 1990 na 1994 na Mashindano ya Uropa ya 1984, 1988 na 1992.

Alitajwa katika timu bora ya michuano hiyo mwaka wa 1984, 1990 na 1992. Pamoja na kushinda mwaka wa 1990, alihusika katika kupoteza fainali za Ujerumani Magharibi dhidi ya Argentina mwaka 1986 na Denmark mwaka 1992.

Bayern Munich walitweet kufuatia habari hyo: ‘FC Bayern wamehuzunishwa sana na kifo cha ghafla cha Andreas Brehme.

‘Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki zake. Andreas Brehme atakuwa katika mioyo yetu milele, kama mshindi wa Kombe la Dunia na, muhimu zaidi, kama mtu maalum sana. Atakuwa sehemu ya familia ya FC Bayern milele. Pumzika kwa amani, Andi!’



Post a Comment

0 Comments