Hatari ya Mlipuko wa Surua,kwa watoto kukosa kinga dhidi ya ugonjwa wa surua

Hatari ya Mlipuko wa Surua,kwa watoto kukosa kinga dhidi ya ugonjwa wa surua

Janga la Uviko -19 lilitatiza utoaji wa chanjo za kawaida dhidi ya ugonjwa wa Surua duniani kati ya mwaka 2020 na 2021 na kuacha mamilioni ya watoto wengi katika nchi maskini, wakiwa hawana kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Kulingana na data za Kituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC), kufikia mwisho wa 2024, zaidi ya nusu ya nchi zote duniani zitakuwa katika hatari ya mlipuko wa Surua.

moja ya magonjwa ya kuambukiza, ambayo yanaweza kusababisha upofu, homa ya mapafu na hata kifo. 

>>Soma Zaidi hapa; Ugonjwa wa Surua,chanzo,dalili,kinga.

Wengi wa watu wanaokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo wa Surua ni watoto. Kabla ya kuanza kufurahia utoto wao, wanakufa kutokana na ugonjwa huu unaoweza kuzuilika kwa urahisi, anasema Abdirizak Ahmed,  mkurugenzi wa shirika la msaada la Save the Children mjini Jijiga nchini Ethiopia ambalo liliripoti kesi 10,000 za ugonjwa huo mwaka 2023, hii ikiwa idadi kubwa zaidi duniani baada ya Yemen, Azerbaijan, Kazakhstan na India. Takwimu hizi ni kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.

Juhudi za Ahmed za kupambana na mripuko wa surua nchini Ethiopia zilipata pigo mwezi uliopita wakati wafanyakazi wenzake wawili walipopoteza watoto wao kutokana na ugonjwa huo, ambao umeibuka tena kutoka barani Afrika kuelekea India na Uingereza.

Watoto hao wote wa kiume walifariki kabla ya kufikisha miezi 13 ama 14 ya maisha yao, hali ambayo Ahmed anasema ni ya kusikitisha.

Watoto 12,000 wafa kwa surua, utapiamlo

Katika kile ambacho wataalamu wa afya wamekiita “kurudi nyuma zaidi katika kizazi kimoja”, nchi 51 – nyingi yao zikiwa barani Afrika – zilishuhudia  miripuko mikubwa na ya kutatiza ya ugonjwa wa Surua mwaka jana, hili likiwa ongezeko kutoka nchi 37 katika mwaka wa 2022 na nchi 22 mwaka 2021, huku hali hiyo ikitarajiwa kuendelea kuwa mbaya zaidi.

Kulingana na data za Kituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC), kufikia mwisho wa 2024, zaidi ya nusu ya nchi zote -takriban 105 – zitakuwa katika hatari kubwa ya mripuko wa ugonjwa wa Surua.

Katika ujumbe wa msemaji wa CDC alioandikia kupitia barua pepe, kati ya nchi zinazokabiliwa na hatari, takribani nusu ni zile zenye mapato ya chini na ya kadri, huku watoto wakikabiliwa na hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo.

Kwa kawaida, ugonjwa wa Surua husababisha homa kali, kikohozi na upele. Miongoni mwa wanawake wajawazito, ugonjwa huo huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba na kuzaliwa mapema kwa mtoto.

Ugonjwa wa surua unaongezeka kufuatia wazazi kutowapa chanjo watoto wao

Ugonjwa wa surua unaongezeka kufuatia wazazi kutowapa chanjo watoto wao.

Hata hivyo, wataalamu wanasema kwa miaka mingi, ufanisi wa chanjo ya Surua umesababisha hali ya kuridhika na sasa idadi inayoongezeka ya wazazi katika nchi ambazo ugonjwa wa Surua ulikuwa umetokomezwa kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na Marekani na Ulaya, wanachagua kutowapa chanjo watoto wao.

Mnamo mwezi Desemba, WHO ilisema kulikuwa na ongezeko la mara 30 zaidi la visa vya ugonjwa wa surua kote Ulaya.

Uingereza, ambayo ilikuwa imeshauangamiza ugonjwa huo mnamo 2017, sasa inajitahidi kudhibiti maambukizo yanayoongezeka kwa sababu ya kupungua kwa idadi ya chanjo inayotolewa.

DR Congo: Vifo kutokana na ugonjwa wa surua vyapindukia 6000

Imani katika umuhimu wa chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa sugu kama Surua na Polio ilipungua wakati wa janga hilo katika nchi 52 kati ya 55 zilizofanyiwa utafiti na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, mwaka 2023.

Niklas Danielsson, mtaalamu mkuu wa chanjo katika shirika la UNICEF, amesema habari potofu kuhusu chanjo za UVIKO- 19

huenda zimesababisha kushuka kwa imani katika chanjo nyingine.

Kulingana na WHO, Surua inaweza kuzuilika kwa dozi mbili za chanjo. Hata hivyo, watoto milioni 22 ulimwenguni kote walikosa dozi yao ya kwanza mnamo mwaka 2022 na wengine milioni 11 dozi yao ya pili, hii ikiwa hatua bora kidogo ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mashirika ya misaada na watalaamu wa afya wanasema kuwa mifumo ya afya barani Afrika iko hatarini haswa kutokana na ukosefu wa fedha na wafanyakazi, hasa katika nchi kama vile Ethiopia ambako migogoro, ukame, mafuriko na utapiamlo kunawafanya watoto kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa hatari.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!