Jikinge na Radi wakati wa Mvua kwa kufanya haya

Mambo ya kuzingatia ili kujikinga na Radi wakati wa mvua.

Radi ni umeme unaotoka katika mawingu na hasa Wingu linaloitwa Wingu Anga ambalo lina barafu ndani yake, inapotokea Wingu na Wingu yanagongana ndipo umeme unapotokea, hali hiyo pia inaweza kuchangia barafu kushuka kwenye ardhi na kuwa mvua inayoitwa ‘Mvua ya Mawe’

Mtaalam na Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (#TMA), Rose Senyagwa anaeleza Umeme wa Radi unaweza kuishia kwenye mawingu kwa maana ya kutoka ulipo kwenda juu au kwenda wingu lingine au kushuka ardhini

Anasema Umeme unaposhuka ardhini unaweza kusababisha madhara kwa viumbe na vitu vingine kwa kuwa mara nyingi Radi huwa inaanza kushambulia vitu virefu vya eneo husika.

Mambo ya kuzingatia ili kujikinga na Radi wakati wa mvua

1. Si Salama kujificha au kujikinga chini ya miti mirefu;

Kwa kawaida uelekeo wa Radi unachagua vitu virefu kuliko vyote katika eneo husika, miti ina uwezo wa kusafirisha umeme,

Hivo epuka kujificha au kujikinga chini ya miti mirefu.

2. Si Salama kujificha chini ya Minara au kwenye kitu chochote kirefu katika eneo husika ikiwemo chini ya nguzo za umeme au Transfoma.

3. Hauruhusiswi kutembea katika maji yanayotiririka au yaliyotuama

Mfano; kwenye dimbwi au maji yanayotembea barabarani,mtoni,Ziwani au katika bwawa,

Kwani maji yanaweza kupigwa na Umeme wa Radi.

4. Haishauriwi kutumia vifaa vya Umeme au vinavyotumia mionzi

Mfano; Simu, Kompyuta, au Laptop, TV, Radio, au Friji kwa kuwa mionzi yake inaweza kuingiliana na Radi.

Hayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kujikinga na Radi wakati wa Mvua.

Chukua Tahadhari…!!!!

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!