Madaktari kote Gaza wanafanya upasuaji kwa wagonjwa bila ganzi

#PICHA:Mwanaume aliyejeruhiwa amelazwa kwenye kitanda katika hospitali ya Gaza European hospital toka mwishoni mwa Disemba.

Madaktari kote Gaza wanafanya upasuaji kwa wagonjwa bila ganzi,

Madaktari wa Gaza wanasema: ‘Tunawaacha wagonjwa wakipiga kelele masaa kwa masaa’.

Madaktari wa Gaza wameelezea jinsi unavyofanyika upasuaji kwa wagonjwa bila ganzi, ili kuwaondoa watu wenye hali sugu, na kutibu majeraha yanayooza kwa vifaa vichache vya matibabu vilivyopo.

“Kwa sababu ya uhaba wa dawa za kutuliza maumivu tunawaacha wagonjwa wakipiga kelele kwa saa na saa,” mmoja aliambia BBC.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeelezea hali ya huduma za afya huko Gaza kuwa ni mbaya sana “wametumia maneno haya(beyond words)”.

WHO; Ilisema hospitali 23 huko Gaza hazifanyi kazi hata kidogo hadi Jumapili – 12 zilikuwa zikifanya kazi kwa kiasi na moja kwa kiwango cha chini sana.

Shirika la afya lilisema mgomo wa anga na ukosefu wa vifaa “umemaliza mfumo ambao tayari hauna rasilimali”.

WHO inasema hospitali ya Nasser, iliyovamiwa na IDF, haifanyi kazi

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema Hamas “kwa chinichini hutumia hospitali na vituo vya matibabu kwa shughuli zake za kigaidi”.

Katika taarifa yake kwa BBC, ilisema IDF “haikushambulia” hospitali, lakini badala yake waliingia katika maeneo maalum… [ili] kuharibu miundo mbinu na vifaa vya Hamas, na kuwakamata magaidi wa Hamas, huku wakifanya kazi kwa tahadhari kubwa”.

IDF Ilisema ilikuwa ikiruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, pamoja na vifaa vya matibabu.

Mashirika ya misaada, ikiwa ni pamoja na WHO, yanasema kumekuwa na “vizuizi vya mara kwa mara vya ufikiaji na kunyimwa kwa huduma”.

Onyo: Makala haya yana maelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kukasirika lakini lengo ni ili kupata Taarifa na kujua hali ya kiafya ilivyo kwa sasa GAZA.

Hii ni kwa mujibu wa Taarifa kutoka WHO, BBC pamoja na mashirika mengine..!!!

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!