Madaktari wa Korea Kusini wagoma, kupinga mpango wa kuongeza madaktari zaidi

Madaktari wa Korea Kusini wagoma, kupinga mpango wa kuongeza madaktari zaidi.

Madaktari walifanya maandamano mjini Seoul wiki iliyopita wakipinga mpango wa serikali wa kuongeza idadi ya madaktari,

Serikali ya Korea Kusini imewaamuru zaidi ya madaktari wadogo 1,000 kurejea kazini baada ya kufanya matembezi mengi kupinga mipango ya kuongeza idadi ya madaktari katika mfumo huo.

Zaidi ya wanafunzi 6,000(interns) na waliokazini walikuwa wamejiuzulu Jumatatu, maafisa walisema.

Korea Kusini ni mojawapo ya nchi zenye uwiano wa chini wa daktari kwa kila mgonjwa kati ya nchi za OECD kwa hivyo serikali inataka kuongeza nafasi zaidi.

Lakini madaktari wanapinga kile wanachohofia kutakuwa na ushindani mkubwa, wachunguzi wa mambo wanasema.

Korea Kusini ina mfumo wa huduma ya afya uliobinafsishwa sana ambapo taratibu nyingi zinahusishwa na malipo ya bima, na zaidi ya asilimia 90% ya hospitali ni binafsi(private hosptal).

“Madaktari wengi wanaamini kutakuwa na ushindani zaidi na kupunguza mapato kwao… ndio maana wanapinga pendekezo la kuongeza Idadi ya madaktari,” alisema Prof Soonman Kwon, mtaalam wa afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Seoul.

Alisema madaktari wadogo wanapinga sera hiyo kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kuathirika mwanzoni mwa kazi zao.

Wizara ya Afya ya Korea Kusini Jumatatu ilisema madaktari 1,630 hawakuwa wamefika kazini Jumanne. Waandalizi walikuwa wameahidi kugoma kuanzia Jumanne.

Hatua hiyo imezua wasiwasi mkubwa kuhusu mfumo wa afya nchini humo wiki hii. Hospitali kadhaa zimehamia kwenye mipango ya dharura.

Matembezi hayo yalipangwa na madaktari wadogo 2,700, ambao ni zaidi ya theluthi moja ya madaktari wanaofanya kazi katika hospitali tano kuu nchini – na ambao ni msingi wa wahudumu wa wodi ya dharura, Yonhap News iliripoti.

Pia kuna hofu kwamba inaweza kusababisha mgomo mkubwa kati ya sekta hiyo – hatua za maandamano zimeidhinishwa na wawakilishi wakuu wa Jumuiya ya Wakazi wa Madaktari wa Korea (Chama cha Daejeon) pamoja na Jumuiya ya Wakazi wa Kikorea.

Madaktari nchini Korea Kusini tayari ni miongoni mwa madaktari wanaolipwa vizuri zaidi duniani, huku takwimu za mwaka 2022 kwa OECD zikionyesha mtaalamu wa wastani katika hospitali ya umma analipwa karibu $200,000 (£159,000) kwa mwaka.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!