Mapacha walioungana wakahesabiwa siku za kuishi wamethibitisha kuwa kila mtu alikosea

Mapacha walioungana wakahesabiwa siku za kuishi wamethibitisha kuwa kila mtu alikosea.

Marieme na Ndeye hawakutarajiwa kuishi kwa zaidi ya siku chache walipozaliwa.

Conjoined twins:

Sasa wana umri wa miaka saba, wanafikiriwa kuwa mapacha pekee wanaokua walioungana barani Ulaya.

Ingawa wasichana hawa wote wana haiba na hisia zao za kipekee, wanategemeana kuishi.

“Hili ndilo nililotaka, wawe na maisha ya kawaida”

“Unapoambiwa tangu mwanzo hakuna wakati ujao, unaishi kwa sasa tu,” baba yao, Ibrahima alisema.

Mapacha walioungana ni nadra, wakiwakilisha takriban mtoto mmoja kati ya kila watoto 500,000 wanaozaliwa wakiwa hai nchini Uingereza.

Takriban nusu huzaliwa wakiwa wamekufa, na wengine watatu hufa ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa.

Kwa hivyo kuona Marieme na Ndeye wakisherehekea siku yao ya saba ya kuzaliwa pamoja na marafiki zao hakumpi Ibrahima furaha tu, bali pia kwa madaktari ambao wamewahudumia.

Ibrahima aliwaweka binti zake Marieme na Ndeye nchini Uingereza kukaa chini ya uangalizi wa matibabu wa Hospitali ya Great Ormond Street

Marieme na Ndeye wana jozi moja ya miguu na fupanyonga moja lakini kila mmoja ana uti wa mgongo na moyo wake.

Wana huduma ya kila saa lakini wanaenda shule ya kawaida huko Wales kusini na marafiki zao.

“Wao ni wapiganaji na wanathibitisha kuwa kila mtu amekosea,” alisema Ibrahima.

“Wanangu wa kike wako tofauti sana, Marieme ni mkimya sana, ni mtu wa kujificha, lakini ni tofauti kabisa na Ndeye, anajitegemea sana.

“NiSingejifanya kuwa ni rahisi lakini ni fursa kubwa. Unajisikia mwenye bahati kushuhudia vita hivi vya kudumu vya maisha.”

Wakati mapacha hao walizaliwa nchini Senegal mwaka wa 2016, wazazi wao walikuwa wanatarajia mtoto mmoja. Madaktari hawakutarajia kuishi kwa muda mrefu zaidi ya siku chache.

“Nilikuwa najitayarisha kuwapoteza haraka sana,” Ibrahima alisema.

“Kitu pekee ambacho tunaweza kufanya ni kuwa kando yao na kutowaruhusu watembee peke yao katika safari hii. Tuliona kwa uwazi mapema sana kwamba tulikuwa tukishughulika na wapiganaji, ambao wanabaki kwenye maisha.” Aliendelea kusema Ibrahima

>>Soma Zaidi hapa Kuhusu: aina hii ya mapacha walioungana;

Conjoined twins:

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!