Putin kuja na Chanjo ya Saratani hivi karibuni

Putin kuja na Chanjo ya Saratani hivi karibuni.

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema wanasayansi nchini humo wanakaribia kutengeneza chanjo ya saratani ambayo itaanza kupatikana hivi karibuni.

Akizungumza jana jioni katika kituo kimoja cha televisheni nchini humo Putin amesema: “tumekaribia sana kuundwa kwa kinachojulikana kama chanjo ya saratani na dawa za kinga za kizazi kipya”.

“Natumai kwamba hivi karibuni zitatumika kwa ufanisi kama njia za matibabu ya mtu binafsi,” aliongeza, akizungumza katika kongamano la Moscow juu ya teknolojia ya siku zijazo.

Putin hakutaja aina gani za saratani ambazo chanjo zilizopendekezwa zingelenga, wala jinsi gani zitafanya kazi.

Idadi ya nchi na makampuni yanafanyia kazi chanjo ya saratani. Mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilitia saini makubaliano na kampuni ya BioNTech yenye makao yake Ujerumani kuzindua majaribio ya kliniki yanayotoa “matibabu ya kibinafsi ya saratani”, yanayolenga kufikia wagonjwa 10,000 ifikapo 2030.

Soma zaidi hapa; Hali ya Saratani Duniani kwa Mujibu wa WHO

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!