Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo la ubongo kumsumbua Wendy Williams



Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo cha Marekani Wendy Williams apatikana na tatizo la ubongo

Nguli wa kipindi cha mazungumzo cha mchana nchini Marekani, Wendy Williams Hunter, aligunduliwa mwaka jana kuwa na aphasia inayoendelea na tatizo la ubongo linalojulikana kama frontotemporal (FTD), timu yake imefichua.

Timu hiyo ilisema ilikuwa ikitoa habari hiyo “ili kurekebisha uvumi usio sahihi na wa kuumiza kuhusu afya yake”.

Bi Williams, umri miaka 59, alikuwa nguli wa kipindi cha Wendy Williams Show kilicho na umaarufu mkubwa kilichokwenda hewani nchini Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja.

Lakini kiliisha mnamo 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.

Habari za kugunduliwa kwa matatizo hayo zinakuja siku moja baada ya jarida la People Magazine, kusema Bi Williams yuko katika kituo cha utunzaji katika eneo lisilojulikana na amekuwa katika hali ya kushangaza ya kiafya.

“Kama mashabiki wa Wendy wanavyofahamu, siku za nyuma amekuwa wazi kwa umma kuhusu mapambano yake ya kimatibabu na Ugonjwa wa Graves’ na Lymphedema pamoja na changamoto zingine muhimu zinazohusiana na afya yake,” timu yake ya utunzaji iliandika katika taarifa Alhamisi.

“Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, maswali yaliibuka wakati fulani kuhusu uwezo wa Wendy wa kuchakata taarifa na wengi wamekuwa wakikisia kuhusu hali ya Wendy, hasa alipoanza kupoteza maneno, kufanya mambo yasio ya kawaidda wakati fulani, na kuwa na ugumu wa kuelewa miamala ya kifedha.”



Post a Comment

0 Comments