Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest)-Benjamin Mkapa

Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest)-Benjamin Mkapa.

IDARA YA MAGONJWA YA DHARURA YA BMH YATIMIZA MIAKA MITANO

Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD) ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imetimiza miaka mitano ya huduma leo.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa BMH,Dkt George Dilunga, amesema Idara hiyo imekuwa ikikuwa na kuongezeka katika utoaji huduma mwaka hadi mwaka. Idadi ya wateja wanaohudumiwa na Idara ya Magonjwa ya Dharura imeongezeka kutoka wateja 1000 kwa mwezi miaka mitano iliyopita mpaka 3500 kwa sasa.

“Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest),” amesema.

Amesema EMD itaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo uokozi katika majanga kama ajali na mafuriko yanayotokeaa sehem mbalimbali nchini.

“EMD ya BMH ilikuwa ni miongoni mwa watoa huduma waliowahi kwenda kutoa huduma Manyara kulipotokea maporoko ya tope yaliyosababishwa na mvua kubwa mwaka jana,” amesema Dkt Dilunga.

Aidha amebainisha kuwa kuna mipango endelevu ya kuhakikisha kuwa huduma bora na za wakati zinaendelea kutolewa idarani hapo ikiwemo kuhakikisha wagonjwa hawakawii kupata huduma za dharura.

Vilevile amebainisha kuwa mipango mingine endlevu ipo kuhakikisha wataalamu zaidi wa magonjwa ya dharura wanapatikana na kupewa mafunzo ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora.

“Tuna mpango pia wa kuendeleza huduma za ambulance (EMS) pamoja na kuweka mfumo mzuri wa uokozi wagonjwa wanaopata dharura za kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest) wawapo hospitalini ujulikanao kama Code Blue” alimalizia Dkt. Dilunga. @wizara_afyatz

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!