Ugonjwa wa ngozi "Psoriasis" Wakata Nywele za Beyonce

Ugonjwa wa ngozi “Psoriasis” Wakata Nywele za Beyonce

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani #Beyoncé, ametaja sababu ya kukatika nywele zake akisema anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaofahamika kama ‘#Psoriasis’.

Kwa mujibu wa Jarida la The People msanii huyo, ameeleza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukimsumbua tangu mwaka 2013.

Amesema ugonjwa huo unatokana na hitilafu katika mwili wa binadamu ambapo chembe hai zinazotengeneza ngozi zinakua haraka kuliko kawaida, matokeo yake ngozi inakuwa na mabaka na nywele kuanza kukatika.

Hata hivyo, msanii huyo mwenye umri wa miaka 42, ameeleza kuwa licha ya kupitia changamoto hiyo anakumbukumbu nzuri ya nywele zake tokea akiwa mtoto namna baba yake alivyokuwa akiziosha na kuzipaka mafuta.

Mbali na hayo, amesema leo Februari 20, katika onyesho lake la ‘#Beyonce’s Formidable Fashion Evolution From Destiny’s Child’, litakalofanyika #Texas nchini #Marekani, atatoa huduma bure kwa watu kuosha nywele zao na kuzipaka mafuta kwa lengo la kukumbuka zake ambazo zimekuwa zikikatika siku hadi siku.

Soma Zaidi hapa kuhusu ugonjwa wa ngozi unaofahamika kama Scalp Psoriasis’.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!