Wapanda mlima Everest kurudi na Kinyesi chao Kambini.
“Milima yetu imeanza kunuka,” Mwenyekiti wa manispa ya Pasang Lhamu, aliiambia BBC,
Watu wanaopanda Mlima Everest sasa watalazimika kusafisha kinyesi chao wenyewe na kukirejesha kwenye kambi ya msingi ili kutupwa, mamlaka imesema,
Kwa sababu ya halijoto kali, kinyesi kinachoachwa kwenye Mlima Everest hakiharibiki kikamilifu.
Kawaida mahema tofauti hujengwa kama vyoo, na mapipa chini ya kukusanya kinyesi lakini wanapoanza safari ya kupanda baadhi ya maeneo huwa na theluji kidogo, kwa hivyo huwalazimu kwenda kwenye choo cha wazi nje.
Ni watu wachache sana wanaorudisha kinyesi chao kwenye mifuko inayoweza kuharibika wakati wa kupanda kilele cha Mlima Everest.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!