Chanjo ya malaria mbioni kutumika nchini Tanzania

Chanjo ya malaria mbioni kutumika nchini Tanzania

Tanzania ipo mbioni kuanza matumizi ya chanjo ya malaria kwa watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano baada ya utafiti wa chanjo mbili kukamilika na kuthibishwa na shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha tatu cha baraza la kutokomeza malaria Tanzania, Kaimu Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria Wizara ya Afya Samwel Lazaro amesema wizara kupitia mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba(TMDA) wako kwenye hatua za kuhakikisha chanjo hizo zinasajiliwa ili iweze kutumika.

“Lazima iwe imesajiliwa ili kujiridhisha ni salama na fanisi tunasubiri mchakato ikamilike nchi iweze kutumia chanjo ya malaria nchi,”amesisitiza.

Akizungumza nasi, Mtafiti wa Masuala ya Malaria na Mkurugenzi wa Sayansi Taasisi ya Afya ya Ifakara Ally Olotu amesema wamefanya tafiti za chanjo mbili ambazo ni RTSs ambayo walianza kufanyia tafiti mwaka 2014 hadi 2019 .

“Tulifanya nchi saba ikiwemo Tanzania tulikuwa Ifakara na NIMR matokeo yalionesha ikuwa salama na iliweza kukinga malaria kali kwa watoto kwa asilimia 30 baadae chanjo ilichukuliwa na kufanyiwa majaribio ya kutumiwa na ikaonekana ni kweli inauwezo wa kukinga kwa asilimia 30 kwa visa vya malaria hai.

Amesema kwa chanjo hiyo ya kwanza WHO iliidhinisha kutumika katika nchi za Afrika zenye malaria za wastani hadi juu.

Kuhusu chanjo ya pili amesema inaitwa R21 ambapo ilifanyiwa utafiti Bagamoyo Mkoa wa Pwani kuanzia mwaka 2021 na vile vile imeonesha ina uwezo wa kukinga kwa watoto wenye chini ya miaka mitano kwa asilimia 70.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!