Inasikitisha! Muigizaji wa vichekesho, Mr Ibu, afariki dunia
Inasikitisha! Muigizaji wa vichekesho, Mr Ibu, afariki dunia
Baada ya kuumwa kwa muda mrefu huku damu ikiganda kwenye mguu wake, mwigizaji mkongwe, John Okafor almaarufu Mr Ibu amefariki dunia.
Muigizaji huyo aliaga dunia katika hospitali moja ndani ya jimbo la Lagos Jumamosi, Machi 2.
Kulingana na vyanzo vya familia, mwigizaji huyo amekuwa akipatiwa huduma(Life support) baada ya kufanyiwa upasuaji wa pili wa maradhi yake hivi karibuni.
Chanzo cha familia kilisema kuwa shinikizo la damu(Blood pressure) liliongezeka zaidi ya 200 baada ya kufanyiwa upasuaji huo na kwamba jitihada zilifanywa ili kuiweka sawa presha hiyo kabla ya kuaga dunia jioni ya Jana.
Muigizaji huyo alipambana na tatizo la kuganda kwa damu mara kwa mara kwenye mguu wake (tatizo linaloathiri mishipa ya damu) na changamoto zingine za kiafya kwa miaka.
Mnamo Oktoba 2023, alijitokeza hadharani kutafuta usaidizi wa kifedha kutibu maradhi yake. Kulikuwa na mipango ya kumsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi lakini mpango huo ulikatizwa na madaktari wake ambao waliamini kuwa haifai yeye kusafiri kwa ndege.
Wakati wa matibabu yake, mguu wake ulikatwa mnamo Novemba 2023.
Muigizaji huyo ameacha mke na watoto. Alikuwa na umri wa miaka 62.
Muigizaji huyo mkongwe alikuwa maarufu sana kwa tafsiri yake nzuri ya majukumu ya ucheshi katika sinema.
Roho yake ipumzike kwa amani, Amina.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!