Ticker

6/recent/ticker-posts

MOI kuwapokea wagonjwa wote wa NHIF hata jumamosi na jumapili



MOI kuwapokea wagonjwa wote wa NHIF hata jumamosi na jumapili.

Na Abdallah Nassoro-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesema imejiandaa vema kuwapokea wagonjwa wote wakiwemo waliokuwa wanatibiwa hospitali binafsi kutokana na hospitali hizo kusitisha kutoa huduma kwa kutumia Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF).

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amebainisha hayo leo Machi 01, 2024 wakati alipokuwa anajibu swali la mteja aliyetaka kujua iwapo MOI inaendelea kutoa huduma kwa kutumia Bima ya NHF.

Amesema Taasisi ya MOI imejiandaa vizuri kuwahudumia wagonjwa hao waliokuwa wakitibiwa hospitali binafsi ambazo wamesitisha huduma za NHIF ikiwa pamoja na kutoa huduma siku za Jumamosi na Jumapili.

“Sisi kama MOI baada ya kuona hayo matangazo kuwa hospitali binafsi zimesitisha huduma za NHIF, sisi kama MOI tutaendelea kuwahudumia wagonjwa wa NHIF kama kawaida, hakuna mgonjwa atakayekosa matibabu kutokana na kitita kipya cha NHIF” amesema Prof. Makubi na kuongeza



Post a Comment

0 Comments