Punguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta pamoja na kufanya mazoezi
Punguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta pamoja na kufanya mazoezi.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito Kwa Watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa Yasisyoambukiza ikiwemo Kisukari na Shinikizo la Juu la Damu (Presha) kwa kupunguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta pamoja na kufanya mazoezi.
Waziri Ummy ametoa wito huo leo Machi 17, 2024 akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika fainali ya Mashindano ya Ishirini na Tatu ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu Kitaifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam.
“Tukizingatia hayo mambo makubwa Matatu, kupumguza matumizi ya sukari, chumvi pamoja na mafuta tutajiepusha na magonjwa mbalimbali Yasiyoambukiza kwa maana magonjwa haya yanaongeza kila siku na yanagharama kubwa sana kuyatibu.” Amesema Waziri Ummy
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!