Kupatwa kamili kwa jua kutashuhudiwa leo katika bara la Amerika Kaskazini
Kupatwa kamili kwa jua kutashuhudiwa leo katika bara la Amerika Kaskazini.
Mwezi utapita mbele ya Jua na kupunguza mwanga wa Jua hadi kutoonekana kwa muda na kuwa giza.
Mamilioni ya watu katika eneo kubwa la Amerika ya Kaskazini watashuhudia kupatwa kwa jua, wakati ambapo mwezi utalifunika kabisa jua kwa zaidi ya dakika nne katika baadhi ya maeneo.
Tukio hilo litashuhudiwa ikiwa hali ya hewa itaruhusu na linatarajiwa kuanzia Mexico, kupitia Marekani hadi Canada. Tukio hili la dakika 4 na sekunde 28 litadumu kwa muda mrefu zaidi ya la mwaka 2017 lililodumu kwa dakika 2 na sekunde 42.
https://www.instagram.com/p/C5f9p2pNV1Y/?igsh=MXNrbHB2eGVodjl1OQ==
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!