Nigeria yaleta chanjo mpya ya 5-in-1 dhidi ya homa ya uti wa mgongo,meningitis
Nigeria yaleta chanjo mpya ya 5-in-1 dhidi ya homa ya uti wa mgongo,meningitis.
Wahudumu wa afya wazindua kampeni ya chanjo inayolenga kuwafikia watu milioni moja
Katika hatua ya kihistoria, Nigeria imekuwa nchi ya kwanza duniani kutoa chanjo mpya (inayoitwa Men5CV) iliyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ambayo inawalinda watu dhidi ya aina tano za bakteria wa meningococcus.
Shughuli za chanjo ya dharura zinafadhiliwa na Gavi, Muungano wa Vaccine, ambao unafadhili hifadhi ya chanjo ya uti wa mgongo duniani kote, na kusaidia nchi za kipato cha chini kwa chanjo ya kawaida dhidi ya homa ya uti wa mgongo.
Nigeria ni mojawapo ya nchi 26 zenye homa ya uti wa mgongo barani Afrika, iliyoko katika eneo linalojulikana kama Ukanda wa homa ya Uti wa mgongo barani Afrika. Mwaka jana, kulikuwa na Zaidi ya asilimia 50% ya visa vya kila mwaka vya homa ya uti wa mgongo iliyoripotiwa kote barani Afrika.
Nchini Nigeria, mlipuko wa serogroup C wa Neisseria meningitidis (meningococcus) ulisababisha visa 1742 vinavyoshukiwa kuwa homa ya uti wa mgongo, ikijumuisha visa 101 vilivyothibitishwa na vifo 153 katika majimbo saba kati ya 36 ya Nigeria (Adamawa, Bauchi, Gombe, Jigawa, Katsina, Yobe, Zamfara) 1 Oktoba 2023 na 11 Machi 2024.
Ili kuzima mlipuko huo hatari, kampeni ya chanjo imefanywa tarehe 25–28 Machi 2024 ili kufikia zaidi ya watu milioni moja wenye umri wa miaka 1-29.
Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi makubwa ambayo husababisha kuvimba kwa utando (meninjis) unaozunguka na kulinda ubongo na uti wa mgongo. Kuna sababu nyingi za ugonjwa wa meningitis, ikiwa ni pamoja na virusi, bakteria, pamoja na vimelea vingine. Dalili mara nyingi ni pamoja na maumivu ya kichwa, homa na shingo kuwa ngumu au kukaza.
Homa ya Uti wa mgongo inayotokana na bakteria ndio mbaya zaidi, Inaweza pia kusababisha tatizo la septicemia na unaweza kulemaza au kuua ndani ya masaa 24 kwa wale wanaougua.
#SOMA ZAIDI HAPA kuhusu Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo,meningitis.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!