Ticker

6/recent/ticker-posts

Njia bora za Kupiga Mswaki na kulinda meno yako na kinywa



Njia bora za Kupiga Mswaki na kulinda meno yako na kinywa

Wengi wetu hatutumii njia bora zaidi za kupiga mswaki, licha ya hatari za kiafya za kushindwa kufanya hivyo.

Kusafisha meno yako kwa ufanisi hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mengi sugu, pamoja na kuweka meno na fizi zako kwenye afya nzuri. Lakini wengi wetu tunafanya vibaya. Hapa kuna njia za jinsi ya kupiga mswaki meno yako vizuri, kulingana na wataalam.

Kwa kawaida wengi wetu tumekuwa tukipiga mswaki kwa mazoea tu pasipo kujua zipi ni njia sahihi za kupiga mswaki,

Nchini Sweden, utafiti mmoja uligundua kuwa Mtu mmoja kati ya 10 ndye anayetumia mbinu bora zaidi ya kupiga mswaki. Bima ya afya ya Uingereza, Bupa iligundua kuwa takriban nusu ya watu waliojibu hawakujua jinsi ya kupiga mswaki ipasavyo katika uchunguzi wa watu 2,000 nchini Uingereza.

“Kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu yeyote ambaye hajapata maelekezo rasmi kutoka kwa daktari wake wa meno au mtaalamu wa usafi anapiga mswaki kimakosa,” anasema Josefine Hirschfeld, profesa mshiriki na mtaalamu wa urejeshaji wa meno katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza. “Kutokana na uzoefu wangu, hii itakuwa idadi kubwa ya watu katika nchi yoyote ile.”

Labda hiyo haishangazi, kwa kuzingatia aina mbalimbali za maudhui zinazopatikana kuhusu jinsi unapaswa kupiga mswaki. Utafiti mmoja ulipata angalau ushauri 66 tofauti, wakati mwingine unaokinzana.

“Nadhani inachanganya sana kwa watumiaji,” anasema Nigel Carter, mtendaji mkuu wa Wakfu wa Afya ya Kinywa nchini Uingereza. Mkanganyiko huu huimarishwa na safu ya bidhaa za meno zinazopatikana kununua, ili mtu atumie kwa ajili ya meno yake.

Ni ipi njia bora ya kupiga mswaki meno yako?

“Wagonjwa wengi wanaelewa kuwa wanachohitaji kufanya ni kuondoa mabaki ya chakula,”. “Hiyo ni kweli kwa kiasi. Ni muhimu zaidi kuondoa bakteria kwenye meno.”

Bakteria hawa na vijidudu vingine hukua ndani ya kinywa cha kila mtu, na kuunda Utando usio na kifani unaojulikana kama “Teeth plaque”.

Inajumuisha takriban spishi 700 tofauti za bakteria, anuwai ya pili kwa ukubwa katika mwili wa binadamu baada ya utumbo, pamoja na kundi la fangasi na virusi. ” Bacteria hawa Wanaishi kwenye utando wa kunata uliokwama kwenye meno na pia kwenye tishu laini,”. “Utando huu wa kunata hauwezi kuoshwa kwa urahisi – inahitaji kusafishwa kwa mikono.”

Sehemu muhimu zaidi ya kuiondoa au kudeal nayo sio kwa kweli meno tu, lakini inaitwa gumline. Hapa ndipo vijidudu vinaweza kupenya vyema kwenye tishu za ufizi na kusababisha uvimbe, na hatimaye hali kama vile periodontitis.

GUMLINE; ni nini?

” Gumline ni ile ncha ya fizi ambapo hukutana na meno “the edge of the gums, where they meet the teeth”. ANGALIA HAPA KWENYE PICHA

Kwa kweli, “kupiga mswaki” ni jambo linalohitaji ujue nini unafanya na sio mazoea tu. “Fikiria kusugua zaidi gumline yako, badala ya meno yenyewe tu, ” Na Meno yatapigika mswaki yenyewe.”

Mbinu za Kupiga Mswaki Vizuri

Hizi hapa ni baadhi ya mbinu za kutumia ili upige mswaki vizuri na kusafisha meno na kinywa kama inavyotakiwa;

1. Bass technique

Mbinu hii inahusisha kuweka brashi ya Mswaki kwa pembe ya digrii 45 kwenye uso wa jino (lililoinamishwa chini kwenye taya ya chini na ya juu, kana kwamba unajaribu kukaribia ukingo chini ya ufizi).

Kisha unafanya harakati ndogo, za mtetemo na kurudi kwenye gumline.

2. Stillman technique

Mbinu hii hufanya kazi nzuri ya kuondoa biofilm. Hapa unakuwa kama unafagia mara kwa mara meno kutoka kwenye gumline, wakati ambapo unaendelea kuangalia maeneo yenye Utando Zaidi uliobaki.

Nguvu,mgandamizo au Shinikizo linalotumika linapaswa kutokuwa zaidi ya 150-400g, Kupiga mswaki kwa nguvu sana, hasa kwa kutumia brashi yenye bristled, kunaweza kusababisha majeraha kwenye ufizi.

Majeraha madogo kwenye tishu laini yanayosababishwa na upigaji mswaki kwa nguvu ni fursa kwa bakteria kuingia kwenye damu.

3. Fones technique

Mbinu hii ni nzuri zaidi kwa watoto na watu wanaoanza kujifunza kupiga mswaki,

Mbinu ya Fones inahusisha kushikilia brashi ya mswaki kwa digrii 90 na kufanya usogezaji wa mviringo juu ya meno, kuruka gumline.

Je,Unatakiwa kusafisha Meno kwa Muda gani?

Kupiga mswaki inatakiwa iwe si chini ya dakika mbili kwa wakati mmoja, mara mbili kwa siku ni pendekezo kutoka Shirika la Madaktari wa Meno la Marekani, NHS, Shirika la Madaktari wa Kihindi, Shirika la Madaktari wa Meno la Australia na mashirika mengine mengi ya kitaifa ya afya.

Shida ni kwamba, wengi wetu ni hawapo vizuri katika kukadiria muda wa dakika mbili kweli. Wastani wa muda ambao tunapiga mswaki hutofautiana kwa kiasi kikubwa, kutoka sekunde 33, sekunde 45 sekunde 46 hadi sekunde 97  kulingana na tafiti mbalimbali.

Takriban 25% tu ya watu hupiga mswaki kwa muda wa kutosha, kwa shinikizo na mwendo sahihi, kulingana na utafiti mmoja ulioongozwa na Carolina Ganss, profesa katika idara ya meno ya kihafidhina na ya kuzuia katika Chuo Kikuu cha Justus-Liebig Giessen nchini Ujerumani.



Post a Comment

0 Comments