Ticker

6/recent/ticker-posts

Tanzania yapiga marufuku dawa ya kikohozi kwa watoto iitwayo Benylin



Tanzania yapiga marufuku dawa ya kikohozi kwa watoto iitwayo Benylin.

Tanzania, Rwanda na Afrika Kusini zimeungana pamoja na Kenya na Nigeria kusitisha matumizi ya dawa ya kikohozi kwa watoto iitwayo Benylin.

Kusitishwa huko kunakuja baada ya vipimo vya maabara nchini Nigeria kubaini kuwa dawa hizo za kikohozi za kampuni ya Johnson & Johnson zilikuwa na sumu.

Dawa hiyo ina kiungo ambacho uchunguzi umebaini kwamba kilisababisha vifo vya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.

Kemikali ya Diethylene glycol ni sumu kwa binadamu inapotumiwa na inaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.

Via:Bbc



Post a Comment

0 Comments