Upasuaji wa kuondoa Jiwe ndani ya kibofu cha Mkojo wafanikiwa

Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuondoa Jiwe ndani ya kibofu cha Mkojo kwa Mwanamke mwenye umri wa miaka 48.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hospitalini hapo jiwe hilo lenye uzito wa Gramu 800 lililomsumbua mhusuka kwa zaidi ya miaka mitatu.

Akizungumza leo Aprili 18, 2024 na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt. Jackson Chiwaligo amesema hiyo ni mara ya kwanza kufanya upasuaji kama huo.

Dkt. Chiwaligo ameeleza kuwa mgonjwa huyo alifika Hospitali ya Sekoutoure akiwa na changamoto ya kupata maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya kibofu cha mkojo ulisababisha kufanyiwa upasuaji na kuondoa lenye uzito wa Gramu 800”, amebainisha Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!