Ticker

6/recent/ticker-posts

Wanaume ‘vinara’ katika uraibu 3,000 wajitokeza kutibiwa MNH



Wanaume ‘vinara’ katika uraibu 3,000 wajitokeza kutibiwa MNH

IDADI ya wanaume waraibu wa dawa za kulevya ni kubwa zaidi, ikilinganishwa na wanawake. Kati ya waliosajiliwa 3,794 kupata huduma saidizi, wanaume ni 3,649 na wanawake ni 145 pekee.

Aidha, kati ya hao 3,794 waliosajiliwa kupatiwa huduma ya matibabu saidizi kwa waraibu wa dawa za kulevya, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hadi Machi mwaka huu, ni 957 pekee, wanahudhuria kliniki ya tiba hiyo MNH.

Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka MNH, Dk. Iddy Haruna, aliyasema hayo, wakati akiwasilisha mada kuhusu huduma hiyo tangu ianzishwe takribani muongo mmoja uliopita, kubaini ilipofikia, changamoto na matarajio.

Mkutano huo, uliandaliwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe kwenye Uzinduzi wa Jumuiya ya Wadau wa Afya ya Akili (ECHO), kwa njia ya mtandao, jana.

Dk. Haruna, alisema miongoni mwa sababu zinazosababisha kuwapo idadi ndogo ya wanaopatiwa huduma hiyo, ikilinganishwa na waliosajiliwa, ni pamoja na wengine wamemaliza tiba, wamefariki, wamehama kituo ama wameacha matibabu.

Aidha bingwa huyo, alisema kuna mahitaji makubwa ya tiba hiyo, pamoja na wataalamu na kwamba hasi sasa idadi ya Vituo vya Tiba Saidizi kwa Kutumia Dawa (Medically Assisted Therapy-MAT), vimefikia 16, kikiwamo kilichopo Gereza la Segerea.

“Waliosajiliwa jumla ni 3,794, kati yo wanaume ni 3,649 na wanawake 145. Wanaopata tiba kwa sasa ni 957. Tunaweza kusema vimefika vituo 16 nikihusisha kilichopo gereza la Segerea, Dar es Salaam na Kihonda, Morogoro.

“Harakati ziko mbioni kufungua satelite (kituo kidogo), kliniki katika wilaya ya Muheza(Tanga) na Chalinze (Pwani),” alisema bingwa huyo.

Alifafanua kwamba, kabla ya kliniki ya MAT, kuanzishwa nchini, kulikuwa ongezeko la Watu Wanaojidunga Dawa za Kulevya (PWID), takriban 50,000 huku wakichangia sindano na kushiriki ngono bila kondomu.

“Maambukizi ya VVU miongoni mwa wadunga sindano yalianza kuongezeka kwa kasi ya kutisha (mara nne ya kiwango cha kitaifa). PWID kwa asilimia 28 ya waliojidunga ni wa kiume na asilimia 62 ni wa kike.

Alivitaja vituo vya MAT ambavyo ni 16 vilivyopo nchini ni MNH; Hospitali ya Rufani ya Mkoa Mwananyamala, Hospitali ya Rufani ya Mkoa Temeke, Hospitali ya Rufani ya Kanda Mbeya, hospitali ya Sekou toure, Mwanza; Hospitali ya Mirembe, Dodoma; Hospitali ya Bagamoyo, Pwani; Hospitali ya  Bombo, Tanga.

Vituo vingine Hospitali ya Tumbi, Pwani; Hospitali ya Mount Meru, Arusha; Kituo cha Afya Tunduma, Songwe; Gereza la Segerea; Kituo cha Afya Tegeta, Dar es Salaam; Zahanati ya Mbagala; Hospitali ya Kigamboni.

HABARI KUU



Post a Comment

0 Comments