WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bure

DAR ES SALAAM; WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bure katika kambi maalum itakayofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Kambi maalum ya upasuaji huo Itafanyika kwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itafanyika Aprili 20 na ya pili mwezi Mei.

Akizungumza leo Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji MOI, Dk Lemeri Mchome amesema wamekuja na mkakati ambao utahakikisha huduma hiyo inawafikia watoto wengi ambao hawajaipata.

“Tumepanga kufanya kambi ya upasuaji tarehe 20 Aprili na Mei, itatanguliwa na kliniki kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa watoto na kuwapanga kwa ajili ya kambi,” amesema.

Amesema MOI kwa kushirikiana na wadau wanafanya huduma hiyo, wakiwemo chama cha wazazi wenye watoto hao na MO Dewji Foundation.

“Kwa niaba ya Watanzania tunawashukuru kwa kuamua kuwasaidia watoto waliopata changamoto, tumeona kwa sasa watoto wapate huduma wote wengine wanakuja na kushindwa kupata matibabu kwa ajili ya fedha tuko na timu nzima kuhakikisha huduma endelevu na jumuishi,”ameeleza.

Mwakilishi wa MO Dewji Foundation, Amina Ramadhani amesema wamepanga kusaidia watoto hao kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

“Kuanzi vipimo na gharama za upasuaji na kufuatilia baada ya huduma na tutawasaidi watoto hawa kwa kipindi cha mwaka tutafatilia hapa MOI na kutoa gharama zote wapate huduma.

Amesema ili kufanikisha hilo watasaidiana kuleta watoto kutoka mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga huku wazazi wakipewa nauli na malazi kwa kushirikiana na ASBATH.

“Kuna watoto ambao wanatoka mikoani kama 25 hivi na wazazi wao hawana uwezo wa kuja, watawezeshwa ili waweze kufika wataandaliwa makazi na ASBATH na tutawasaidia kupata chakula.

Aidha MKurugenzi wa Chama cha Wazazi wa Wwatoto Wenye ulemavu wa Kichwa kikubwa na Mgongo wazi(ASBATH), Suma Mwaipopo amewashukuru wote kwa ushirikiano kwa ajili ya kambi na kuwasihi wazazi kutoka mikoa yote wasikose kwa faida yao.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!