Historia:Mvumbuzi wa kwanza wa Taulo za kike (pads)

Historia:Mvumbuzi wa kwanza wa Taulo za kike (pads)

Huyu ndio Mwanamke wa kwanza kugundua taulo za kike

Maisha ya sasa siyo sawa na ya zamani, wakati mwaka 1920 wanawake walikuwa wakipata wakati mgumu unapokuja wakati wa siku zao za mzunguko za hedhi, huku baadhi yao wakitumia vitambaa kujistiri, lakini alitokea mkombozi ambaye aliwapa matumaini ya kufanya wanawake kujiamini tena kwa kuvumbua Taulo za kike (pads) ambazo zingewasaidia.

Mary Beatrice Kenner mwenye asili ya Afrika alizaliwa Mei 17, 1912 North Carolina, alikuwa ni mzaliwa katika familia ya wavumbuzi ambapo baba yake mzazi Sidney Nathaniel Davidson, aliwahi kugundua baadhi ya vifaa mbalimbali vya mawasiliano kwa miaka hiyo.

Baada ya kuhitimu shule yake ya upili ya ‘Paul Lawrence Dunbar’ ndipo alifanikiwa kwenda kusoma katika ‘Chuo Kikuu cha Howard’, kwakua alikuwa na changamoto za kifedha hakuweza kuendelea na masomo ndipo akaamua kuanzisha biashara ya kuuza maua ambapo alifanikiwa kumiliki maduka manne ya Maua huku akiendelea kuunda uvumbuzi wake wa taulo za kike.

Aliendelea kutengeneza taulo hizo huku akiwa anawauzia baadhi ya watu waliokwenda kununu maua dukani kwake mpaka ilipofikia mwaka 1956 ambapo alikabidhiwa hati miliki ya uvumbuzi wa taulo hizo alizozipa jina la ‘Sanitary Belt with Moisture Proof Napkin Pocket’ zenye muonekano kama nguo ya ndani ya lastiki ambayo katikati aliweka kitamba ambacho kinauwezo wa kuhimiri damu sitoke kwenye nguo.

Kutokana na kupata hati miliki hiyo kampuni ya Sonn-Nap-Pack ilivutiwa kufanya kazi na mwanadada huyo ambaye alikuwa na matumaini makubwa kuwa angeweza kununua nyumba na gari lakini matumaini hayo yalipotea baada ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo kugundua kuwa #Kenner alikuwa Mwafrica waliamua kusitisha mpango wa kufanya naye biashara.

Hatimaye, bila mshirika wa kufadhili bidhaa yake, aliamua kuendelea kufanya marekebisho katika taulo aliyoizindua huku lengo lake likiwa kurahisisha maisha kwa wanawake wakati wa hedhi lakini kwa bahati mbaya zaidi licha ya kuvumbua kitu ambacho kinasaidia dunia nzima hakuwahi kuwa tajiri, kupata Tuzo yoyote wala kutambulika rasmi kuwa alikuwa mvumbumbuzi wa taulo za kike.

Januari 13, 2006 #MaryBeatriceKenner alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 93 huku mchango wake katika historia ya uvumbuzi ikiwa imepuuzwa kwa kiasi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!