nor 5 inatibu nini,Soma hapa kuifahamu Norethindrone

nor 5 inatibu nini

Dawa hii inajulikana pia kama Nor N 5mg Tablet au Norethindrone,

Dawa hii mara nyingi hutumika kutibu aina mbali mbali za matatizo ya hedhi ikiwemo; maumivu wakati wa hedhi,kuvuja damu nyingi,periods kutokueleweka, tatizo la premenstrual syndrome (PMS), au matatizo kama vile endometriosis n.k.

Dawa hii imetengenezwa na binadamu kutoka kwenye vichocheo asilia vya mwili ambavyo hujulikana kama progesterone(sex hormone progesterone).

Norethindrone huweza kutumika kutibu mwanamke mwenye tatizo la kuvuja damu kutoka kwenye kizazi  yaani “abnormal bleeding from the uterus”.

Pia huweza kutumika ikiwa mwanamke ameacha kupata Hedhi yake kwa miezi kadhaa wakati sio mjamzito au hayupo kwenye kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause), tatizo ambalo hujulikana kama (amenorrhea).

Aidha, dawa hii hutumiwa kutibu hali ya (endometriosis) ambapo tishu ambazo kwa kawaida huwekwa ndani ya uterasi hupatikana nje ya uterasi kwenye eneo la tumbo / pelvic, na kusababisha maumivu / vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida.

Norethindrone ni aina ya hormone (progestin).Ni kama homoni ya progesterone ambayo mwili wako hutengeneza kwa kawaida. Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa kawaida wa ukuta wa uterasi wakati wa mzunguko wa hedhi na kuashiria mabadiliko ya homoni kwenye uterasi ili kurejesha hedhi ya kawaida.

NB: Dawa hii haipaswi kutumiwa ili upate ujauzito. Projestini hazifanyi kazi katika kuzuia kuharibika kwa mimba.

jinsi ya kutumia dawa ya Norethindrone

Tablets;Dawa hii hutumika kwa mdomo kama ilivyoagizwa na daktari wako. Unaweza kuitumia pamoja na chakula au baada ya chakula ili kuzuia usumbufu wa tumbo. Fuata kwa uangalifu dose sahihi ya dawa. Uliza daktari wako ikiwa una maswali yoyote. Dose ya dawa hutegemea hali yako ya matibabu na majibu ya matibabu.

Kwa matibabu ya kusimamishwa kwa hedhi na kutokwa na damu isiyo ya kawaida kutoka kwenye uterasi, Tumia dawa hii kama ilivyoelekezwa na daktari wako, kwa kawaida hutumika mara moja kwa siku kwa siku 5 hadi 10 katika nusu ya pili ya mzunguko wa hedhi uliopangwa. Kutokwa na damu kwa kawaida hutokea ndani ya siku 3 hadi 7 baada ya kuacha kutumia dawa.

Maudhi ya Dawa(Side Effects)

Dawa hii ya Norethindrone huweza kusababisha;

  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kichwa kuuma
  • Kizunguzungu
  • Mood kubadilika
  • Kukosa Usingizi
  • Uzito kuongezeka
  • Uzito kupungua
  • Chunusi kwenye ngozi
  • Matiti kuuma
  • Matati kuvimba
  • Kubadilika kwa hamu ya tendo
  • Ukuaji wa nywele usiowakawaida
  • Nywele kupotea au kunyonyoka n.k

Kumbuka dawa hii hutumika pale ambapo imeonakana Faida ni kubwa kuliko madhara kwa mgonjwa, Na watu wengi hutumia dawa hii pasipo kupata madhara makubwa.

Hakikisha unaongea na wataalam wa afya ikiwa unapata madhara makubwa kama vile;

– Kuvuja damu ukeni

– Kubadilika kwa hedhi,hali ambayo hukuwa nayo

– Kukosa kabsa hedhi,

– Kutokwa na uchafu usio wakawaida ukeni

– Kuvimba miguu au mikono

– Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa

– Ngozi kubadilika rangi na kuwa manjano

– Kuwa na Alama nyeusi kwenye ngozi au Uso(dark patches on the skin or face (melasma).n.k

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!