Plasmolifting: Jinsi wanawake walivyoambukizwa VVU Marekani wakati wa kupodolewa nyuso zao

Plasmolifting: Jinsi wanawake walivyoambukizwa VVU Marekani wakati wa kupodolewa nyuso zao

Maelezo ya picha,Inaaminika kuwa hiki ndio kisa cha kwanza nchini Marekani kutokea wakati wagonjwa waliambukizwa VVU wakati wa kutumia vipodozi.

Habari za hivi punde kwamba wanawake nchini Marekani walipata virusi vya Ukimwi (VVU) wakati wa utaratibu wa kuinua maji ya damu au plasma zilizua maswali kuhusu usalama wa baadhi ya taratibu za urembo.

Kulingana na ripoti ya Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), angalau wanawake watatu waliambukizwa kwenye saluni ya urembo(spa) huko New Mexico mnamo 2018. Ripoti hiyo pia inasema kuwa visa hivi vinatoa mwanga juu ya njia mpya za kueneza maambukizi.

Hii inaaminika kuwa haya ni maambukizi ya VVU ya kwanza kabisa yanayohusiana na utaratibu wa urembo yaliyoyorekodiwa nchini Marekani.

Je, kuinua plasma ni nini na jinsi gani wanawake waliambukizwa VVU wakati wa utendaji wake? Watu wanaweza kufanya nini ili kujilinda kutokana na maambukizi wakati wa taratibu za vipodozi?

Tunaelezea kile kinachojulikana kuhusu hilo na kile wataalam wanachosema.

Kuinua plasma ni nini

Plasmolifting, au PRP (Platelet Rich Plasma) ni utaratibu wa kawaida wa vipodozi, wakati ambapo mgonjwa hudungwa maji ya damu (plasma) yenye damu yake mwenyewe. Kwa kuwa utaratibu unahusisha vitendo na damu, wakati mwingine huitwa “Dracula therapy”.

Wakati wa utaratibu huu , daktari huchukua damu kutoka kwa mshipa wa mtu, hutumia kifaa maalum kinachotumiwa kutenganisha vimiminika vya mwili (centrifuge) ili kutoa maji ya damu kutoka humo, na kisha kuiingiza chini ya ngozi kwa kutumia sindano nyembamba.

Inaaminika kuwa utaratibu huo unaboresha michakato ya kuzaliwa upya (rejuvenation) kwa ngozi, na kuchochea uzalishaji wa collagen mpya na uwezo wa ngozi kutanuka. Inaweza kupunguza kuonekana kwa makunyanzi au makovu ya upele wa mwili.

Utaratibu huo umejulikana kwa miaka mingi. Nyuma mnamo 2013, nyota wa filamu za maisha halisi Kim Kardashian alionyesha uso wake baada ya kufanyiwa utaratibu huo kwenye Instagram.

Hata hivyo, miaka michache baadaye, Kardashian alisema kwamba hatafanya tena utaratibu huu kwa sababu ulikua “mgumu na ulionisababishia maumivu.”makali.

Utaratibu kawaida huchukua dakika 40.

Jinsi gani wanawake wa New Mexico walipata VVU?

Katika majira ya joto ya 2018, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani kilifahamu kuhusu mwanamke wa Marekani mwenye umri wa miaka kati ya 40-50 ambaye alipimwa na VVU akiwa nje ya nchi.

Mwanamke huyo aliripoti kwamba hakutumia dawa za sindano, hakutiwa damu kwenye mishipa hivi majuzi, na hakuwa na mahusiano ya kingono na mtu mwingine yeyote isipokuwa mpenzi wake wa sasa.

Lakini alifichua kuwa alifanyiwa utaratibu wa kuinua uso kwa njia ya kuongezewa plasma kwenye kituo kimoja cha mapodozi huko New Mexico mapema mwaka huo.

Uchunguzi wa CDC uligundua kuwa kituo hicho (spa), ambayo pia ilitoa huduma zingine za sindano kama sindano za Botox (kuongeza makalio) haikuwa na leseni na ilitumia “taratibu zisizo salama za kudhibiti maambukizi.”

Katika jumba hilo, walipata “mirija ya damu isiyo na lebo na sindano za matibabu” zilizohifadhiwa kwenye jokofu la jikoni karibu na chakula, pamoja na “sindano zisizofunikwa” zilizotawanyika ndani ya kabati na kwenye kwenye meza ya mapokezi.

Baadhi ya bakuli za damu pia zilionyesha dalili za kutumika tena, na CDC ilipata angalau mteja mmoja ambaye alipimwa na kuambukizwa VVU kabla ya kutembelea kituo cha matibabu.

Tangu wakati huo, shirika hilo la afya limehusisha kituo hicho na visa vitano vya maambukizi ya VVU, wakiwemo wanawake wanne ambao walifanyiwa taratibu za kuinua nyuso zao kwa kutumia maji ya damu kati ya miezi ya Mei na Septemba mwaka 2018, pamoja na mwanamume ambaye alikuwa katika uhusiano na mmoja wa wanawake hao.

Kulingana na CDC, kwa mwanamume na mwanamke katika uhusiano walioonekana kuwa na maambukizi ya VVU ya hatua ya mwisho walikuwa walipata maambukizi hayo kabla ya kufanyiwa utaratibu huo wa uso.

Kituo hicho cha urembo (Spa) kilifungwa mwishoni mwa 2018, na mmiliki wake wa zamani, Maria de Lourdes Ramos De Ruiz mwenye umri wa miaka 62, anatumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu jela. Mnamo 2022, alikiri kufanya utaratibu hu owa matibabu ya urembo bila leseni.

Je, taratibu hizi ni salama?

Mamia ya nyaraka na tafiti za matibabu zilizochapishwa zinaonyesha kuwa kuinua plasma ni bora katika kutibu majeraha ya michezo, chunusi, eczema na hali nyingine za ngozi.

Chama cha Chuo cha Marekani cha tiba ya ngozi kinasema utaratibu yenyewe, ikiwa unafanywa kwa usahihi, ni salama.

“Baadaye, unaweza kupata maumivu kwenye eneo ulipochomwa sindano, pamoja na michubuko kidogo na uvimbe,” shirika linasema athari “Hizi kawaida hupotea ndani ya siku chache.”

Hatari kubwa zaidi inahusiana na jinsi damu inavyochakatwa na kituo kinachotoa matibabu.

“Ni muhimu kwamba damu iliyochukuliwa kutoka kwa mwili wako ni salama. Vinginevyo, unaweza kupata maambukizi,” chama kinasema.

Pia ni muhimu kuhakikisha kwamba damu iliyorudishwa ni ya mteja na si ya mtu mwingine, vinginevyo mpokeaji anaweza kuwa mgonjwa sana.

Wataalamu wanasema kwamba wale wanaotaka kupata matibabu ya urembo wanapaswa kuhakikisha mapema kwamba saluni ina leseni. Pia wanapaswa kuzingatia jinsi wafanyakazi wanavyoshughulikia vifaa vya matibabu kama vile sindano.

Kuinua plasma sio matibabu pekee ya vipodozi ambayo hivi karibuni yamefanya ambayo yamego nga vichwa vya habari kuhusiana na kusababisha magonjwa mabaya.

Maafisa wa afya wa Marekani walionya wiki iliyopita juu ya mlipuko wa ugonjwa wa botulism unaohusishwa na uongezaji gushi wa makalio ambao umepelekea watu 22 kuugua katika majimbo 11, ambao baadhi yao bado wamelazwa hospitalini.

Botulism ni ugonjwa mbaya ambao husababisha kupungua kwa uwezo wa kuona, ugumu wa kumeza na kupumua, na kushindwa kuongea na uchovu.

Sindano za Botox ni utaratibu maarufu unaotumiwa kulainisha mikunjo na kufanya ngozi ionekane changa. Sindano kawaida hugharimu takriban $530 kwa matibabu.

Kama ilivyo kwa kuinua maji ya damu (plasma), CDC inawashauri wale wanaopenda kufanyiwa tiba ya sindano za Botox kutafiti mtoa huduma kabla na kuhakikisha kuwa Botox ambayo mtaalamu wa urembo anaitumia imeidhinishwa na kununuliwa kutoka kwa chanzo kinachotegemewa.

Via:BBC

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!