Prednisolone inatibu ugonjwa gani?

Prednisolone inatibu ugonjwa gani

Matumizi ya dawa aina ya Prednisolone yameongezeka sana kwa hivi sasa, Dawa hizi ni jamii ya STEROIDS ambazo hutumika kutibu matatizo mbali mbali kwa binadamu kama vile;

• Aina mbali mbali za Allergies(mzio)

• Vimbe mbali mbali mwilini yaani Inflammatory conditions

• Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases

• Aina mbali mbali za kansa au saratani

• Tatizo la Adrenocortical insufficiency

• Kiwango kikubwa cha Calcium kwenye Damu

• Ugonjwa wa Rheumatoid arthritis

• Magonjwa ya ngozi kama vile Dermatitis

• uvimbe kwenye macho

• Tatizo la Multiple Sclerosis,Asthma

• Pamoja na magonjwa mengine mengi

MATUMIZI ya PREDNISOLONE

– Dawa hizi za Prednisolone zipo katika mifumo mikuu minne(4) yaani;

1. Kuna Prednisolone ya VIDONGE vya kunywa Mdomoni(Prednisolone Tablets)

2. Kuna Prednisolone ya SINDANO(Prednisolone Intravenous{IV} Injection)

3. Kuna Prednisolone CREAM ya kupaka kwenye ngozi(Prednisolone Topical Cream)

4. Na kuna Prednisolone MATONE YA MACHO yaani(Eye drops)

#SOMA Zaidi hapa kuhusu PREDNISOLONE

SIDE EFFECTS ZA DAWA YA PREDNISOLONE

– Aina hii ya dawa huweza kuleta maudhi mbali mbali kwa mgonjwa baada ya matumizi kama vile;

✓ Kuleta kichefuchefu

✓ Kusababisha mwili kuchoka kuliko kawaida

✓ Matatizo ya Figo kwa baadhi ya wagonjwa kama ikitumiwa kwa muda mrefu

✓ Matatizo ya akili japo ni kwa asilimia 5% ya wagonjwa

✓ Matatizo ya mifupa ikiwa ni pamoja na mifupa kukosa nguvu n.k

✓ Mgonjwa kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa kama Yeast infection(Fangasi,Uti,Pid N.k) kutokana na shida ya kushuka kwa kinga ya mwili

✓ Kupatwa na tatizo la Kiungulia yaani Heartburn

✓ Kupatwa na Maumivu makali ya kichwa

✓ Kupatwa na tatizo la kizunguzungu kikali

✓ Mzunguko wa hedhi kubadilika kabsa kwa Wanawake

✓ Kupatwa na tatizo la kukosa usingizi

✓ Kuvuja jasho kupita kawaida

✓ Ngozi kuanza kuwa na chunusi,vijibu vidogo N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!