Sindano ya kupunguza uzito 'inaweza kupunguza mshtuko wa moyo'

Sindano ya kupunguza uzito ‘inaweza kupunguza mshtuko wa moyo

Sindano iliyoundwa kukabiliana na unene wa kupindukia inaweza kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi kwa watu bila kujali kiwango cha uzito wanachopoteza wakati wa kutumia dawa hiyo, kulingana na utafiti mpya.

Watafiti waliangalia athari za semaglutide, ambayo ni dawa iliyoagizwa na daktari ambayo inapunguza hamu ya kula na inauzwa chini ya majina ya chapa Wegovy, Ozempic na Rybelsus.

Walisema sindano ya kupambana na unene kupindukia inaweza pia kusaidia afya ya moyo na mishipa ya mamilioni ya watu wazima.

Prof John Deanfield, ambaye aliongoza timu ya watafiti, alisema dawa hiyo ya asili inaweza kuwa na athari chanya kwenye sukari ya damu, shinikizo la damu au uvimbe, pamoja na athari za moja kwa moja kwenye misuli ya moyo na mishipa.

Utafiti wa miaka mitano wa Chuo Kikuu cha London (UCL) ulitumia data kutoka kwenye jaribio linaloendeshwa na semaglutide Novo Nordisk, kuchunguza watu wazima 17,604 zaidi ya umri wa 45 kutoka nchi 41.

Akizungumza kabla ya kuwasilisha utafiti huo katika Kongamano la Ulaya kuhusu Unene wa Kupindukia (ECO) huko Venice, Prof Deanfield alisema matokeo hayo yalikuwa na “athari chamga za kiafya”.

Alisema ulikuwa ugunduzi muhimu, akiufananisha na wakati statins zilianzishwa katika miaka ya 1990.

“Hatimaye tuligundua kuwa kulikuwa na dawa ambazo zilibadilisha biolojia ya ugonjwa huu kufaidisha watu wengi. Hayo yalikuwa mafanikio makubwa.

“Sasa tuna aina hizi za dawa ambazo pia zinaweza kusaidia magonjwa mengi sugu ya uzee.”

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!