Tatizo la Mdomo Sungura kwa watoto husababishwa na nini?

Tatizo la Mdomo Sungura kwa watoto husababishwa na nini?

Tatizo la Mdomo sungura ambapo kwa kitaalam hujulikana kama cleft lip and  palate ni aina ya ulemavu ambao chanzo chake ni sehemu ya uso na mdomo kushindwa kufunga wakati wa uumbaji wa mtoto akiwa tumboni.

Tatizo la mdomo sungura mara nyingi hutokea katika wiki ya tano hadi ya nane ya ukuaji wa mtoto anapokua tumboni ambapo sehemu tatu za uso yaani sehemu ya juu, pembeni na chini hushindwa kukutana,

Tatizo hili huwapata baadhi ya watoto bila kujali jinsia yao.

CHANZO CHA MDOMO SUNGURA NI NINI?

Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kujua sababu halisi ya mtoto kuzaliwa na hali hii ila Zipo sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa watoto kuzaliwa na tatizo la Mdomo sungura, na sababu hizo ni kama vile;

– Sababu ya Kigenetic, hapa huhusisha uwepo wa Vinasaba vya tatizo hili la Mdomo Sungura

– Mama mjamzito kunywa Pombe kupita kiasi,Unywaji pombe kipindi cha ujauzito huweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto wako aliyetumboni

– Mama mjamzito kuvuta Tumbaku,Sigara,pamoja na matumizi ya Ugoro kipindi cha ujauzito.

– Tatizo la kupata Lishe duni kwa mama mjamzito, hali ambayo hupelekea mama mjamzito kukosa virutubisho muhimu kama vile vitamini,foliki asidi n.k.

virutubisho hivi ni muhimu sana kwenye uumbaji wa uti wa mgongo, ubongo,mfumo mzima wa fahamu pamoja na maeneo mengine ya mwili wa mtoto kama vile Uso n.k.

– Matumizi ya baadhi ambazo haziruhusiwi kwa mama mjamzito,hasa katika miezi mitatu ya kwanza,ambapo uumbaji wa viungo mbali mbali vya mtoto hufanyika yaani Organogenisis.

MATIBABU YA TATIZO HILI LA MDOMO SUNGURA

Tiba kubwa ya tatizo hili ni UPASUAJI, Watoto wenye ulemavu huu wa mdomo Sungura hufanyiwa upasuaji na kurudisha viungo vilivo athirika katika hali yake ya kawaida.

MAELEKEZO ZAIDI,Soma hapa:

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!